Mhandisi Mramba na JICA wajadili utekelezaji wa Miradi ya Nishati

Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba amekutana na Wataalam kutoka Shirika la Maendeleo la Japan (JICA) ili kujadili hali ya utekelezaji wa miradi ya Nishati inayofadhiliwa na shirika hilo kwa lengo la kuhakikisha kuwa miradi hiyo inatekelezwa kwa wakati na kwa ufanisi.

Kikao hicho kimefanyika Septemba 8, 2025 katika ofisi za Wizara ya Nishati Mtumba Jijini Dodoma ambapo pande hizo mbili pia zilijadiliana kuhusu suala la kujengea uwezo wataalam wa Wizara ya Nishati, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) katika masuala ya kusanifu mitandao ya usambazaji wa Gesi Asilia.

Miradi iliyojadiliwa kwa kina katika kikao hicho ni wa kusafirisha umeme kutoka Tanzania hadi Uganda (UTIP) na mradi wa umeme Dodoma Ring Circuit unaolenga kuzidi kuimarisha hali ya upatikanaji umeme Dodoma.

Katika kikao hicho, Mha. Mramba ameisisitiza JICA kuhusu suala la utekelezaji mradi wa mfano wa usambazaji gesi asilia katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma ambao utakuwa kielelezo cha manufaa ya gesi asilia iliyogunduliwa hapa nchini ambayo itasaidia pia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Vilevile, Mramba ameishukuru JICA kwa kufadhili miradi ya Nishati ambayo imekuwa chachu ya maendeleo nchini hususan katika Jiji la Dodoma ambalo linaendelea kukua kwa kasi.

spot_img

Latest articles

Mnyama Simba afia kwa Mkapa, Yanga, Azam kicheko

Na Winfrida Mtoi LIGI Kuu Tanzania Bara imeendelea leo Novemba 7, 2025 kwa michezo miwili...

Waziri Aweso aweka kambi Dar kupambana na changamoto upungufu wa maji

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso (Mb) amefanya ziara ya kikazi katika...

Waziri wa Nishati Ndejembi azindua rasmi mita janja

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amezindua rasmi mita janja (smart meter)...

RC Kunenge: Mto Ruvu ubaki kwa matumizi ya binadamu tu, tusitishe shughuli nyingine kwa muda

Na Mwandishi Wetu MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ametoa wito kwa wakulima...

More like this