Rais Mwinyi akagua Mji wa AFCON Fumba

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, ametembelea mradi wa Mji wa AFCON – 2027 Fumba uliopo Mkoa wa Mjini Magharibi, pamoja na kukagua uwanga unaotarajia kutumika kwa michuano hiyo

Ziara hiyo imefanyika leo  Aprili 14, 2026, akiambatana na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Riziki Pembe Juma, pamoja na wadau wa mradi wa AFCON Fumba.

Katika ziara hiyo, Rais Mwinyi amekagua maeneo mbalimbali ya uwanja huo, unaotarajiwa kutumika kwa michuano ya AFCON mwaka 2027 itakayofanyika kwa ushirikiano wa nchi tatu za Afrika Mashariki za Kenya, Uganda na Tanzania.

Aidha, ametembelea na kukagua miundombinu inayotarajiwa kujengwa kuzunguka uwanja huo, ikiwemo hospitali, barabara, migahawa, maduka makubwa (mall) pamoja na huduma nyingine muhimu zitakazouzunguka mji huo wa kisasa.

Uwanja huo unakadiriwa kuchukua watazamaji elfu 35, ukiwa na viwango vya ubora vinavyokubalika na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).

spot_img

Latest articles

Sowah apigwa faini nzito  kwa utovu wa nidhamu, ashushwa U-20

Na Winfrida Mtoi UONGOZI wa Klabu ya Simba umeweka wazi hatua kali za kinidhamu zilizochukuliwa...

Waziri Mavunde aelekeza kusimamishwa kwa shughuli za uchimbaji Busulwangili-Kahama – Kahama

Na Mwandishi wetu, Dodoma WAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde, ameagiza kusimamishwa mara moja kwa...

DC Mkude akabidhi vyombo vya usafiri Tanesco Mkoa wa Arusha kuimarisha utoaji huduma

📌 Ni katika muendelezo wa mkakati wa TANESCO wa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi. 📌...

DCEA yakamata Kilo 101.2 za Mirungi ndani ya Basi la Abood, watano mbaroni

Na Mwandishi wetu Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata...

More like this