Rais Mwinyi atembelea Banda la ETDCO Sabasaba

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, leo 7 Julai 2025, ametembelea banda la Kampuni ya ETDCO katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa, Dar es Salaam na kujionea namna Kampuni hiyo inavyotekeleza miradi mbalimbali ya umeme nchini.

Akiwa katika banda hilo, Rais Dkt. Mwinyi amekabidhi zawadi ya sikukuu ya Sabasaba kwa wafanyakazi wa ETDCO wakiongozwa na Kaimu Meneja wa Kampuni hiyo, CPA. Sadock Mugendi.

Akizungumza na kuhusu na ushiriki wao katika maonesho hayo, CPA. Mugendi amesema kuwa lengo la ETDCO kushiriki meonesho ya sabasaba ni kuonesha utekelezaji wa Miradi mbalimbali ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya umeme nchini.

CPA Mugendi ameeleza kuwa Kampuni hiyo imefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya usafirishaji umeme, ikiwemo mradi wa kusafirisha umeme wa kilovolti 132 kutoka Tabora hadi Katavi, ambao umewezesha wananchi wa maeneo hayo kupata umeme wa uhakika.

Aidha, amebainisha kuwa wameweza kukamilisha mradi mwingine wa kilovolti 132 kutoka Tabora Mjini hadi Urambo, wenye urefu wa kilomita 115, umeendelea kuimarisha upatikanaji wa umeme katika Mkoa huo.

“Tunawakaribisha wananchi wote kutembelea banda letu la ETDCO lililopo ndani ya banda la TANESCO. Lengo letu ni kuwaonesha wadau namna tunavyotekeleza miradi mbalimbali ya umeme kwa lengo la kuhakikisha watanzania wanafikiwa na huduma nchi zima,” amesema CPA. Mugendi.

Ameongeza kuwa kampuni hiyo imefanikiwa kutekeleza miradi ya REA katika Mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Arusha, Katavi, Mbeya, Geita, pamoja na Kigoma.

CPA. Mugendi ameeleza kuwa utekelezaji wa awamu ya pili ya mradi wa kusafirisha umeme kutoka Urambo – Nguruka – Kigoma, utakuwa wa kilovolti 132 wenye urefu wa kilomita 260.

Ameongeza kuwa mafanikio haya ni matokeo ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita, inayolenga kuhakisha watanzania wanafikiwa na huduma bora ya umeme nchini.

spot_img

Latest articles

Tume Jaji Chande imekwepa kututajia aliyekutwa na ngozi ya ng’ombe

NINGALI ninaitafakari ripoti ya Jaji Mohammed Chande ya matukio ya Oktoba 2025 wakati na...

Adaiwa kumuua mtalaka wake kwa panga kisa nguvu za kiume

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi mkoani Lindi linamshikilia Hassan Athuman Mpogo (46), mvuvi na...

Rais Ruto kuhutubia Bunge Tanzania

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Kenya, William Ruto, anatarajiwa kuhutubia Bunge la Tanzania Mei 5,...

Mwigizaji, msanii wa Bongo Flava wafariki dunia

Na Mwandishi Wetu MSANII wa filamu nchini, Hashim Kambi, amefariki dunia leo alasiri akiwa anapatiwa...

More like this

Tume Jaji Chande imekwepa kututajia aliyekutwa na ngozi ya ng’ombe

NINGALI ninaitafakari ripoti ya Jaji Mohammed Chande ya matukio ya Oktoba 2025 wakati na...

Adaiwa kumuua mtalaka wake kwa panga kisa nguvu za kiume

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi mkoani Lindi linamshikilia Hassan Athuman Mpogo (46), mvuvi na...

Rais Ruto kuhutubia Bunge Tanzania

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Kenya, William Ruto, anatarajiwa kuhutubia Bunge la Tanzania Mei 5,...