Adaiwa kumuua mtalaka wake kwa panga kisa nguvu za kiume

Na Mwandishi Wetu

JESHI la Polisi mkoani Lindi linamshikilia Hassan Athuman Mpogo (46), mvuvi na mkazi wa Kata ya Somanga wilayani Kilwa, kwa tuhuma za kumuua kwa kumkata na panga mke wake wa zamani, Aisha Mkimbizi (41), mjasiriamali wa biashara ya samaki.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, ACP John Imori,  mtuhumiwa alitekeleza tukio hilo baada ya kuamini taarifa alizopewa na mganga wa kienyeji kuwa marehemu alikuwa akimloga na kusababisha kuishiwa nguvu za kiume.

Amesema tukio hilo lilitokea Aprili 26, saa 12 asubuhi, wakati marehemu akitoka Somanga kuelekea baharini kwa shughuli zake za biashara ya samaki. Inadaiwa mtuhumiwa alimvamia na kumkata kwa mapanga, hali iliyosababisha kifo chake akiwa njiani kupelekwa kituo cha afya.

Jeshi la Polisi linamshikilia pia mganga wa kienyeji, Haji Said Nguvunze (46), mkazi wa Somanga, ambaye amekiri kumweleza mtuhumiwa kuwa mke wake waliyetalikiana ndiye anayemloga.

Polisi wametoa wito kwa wananchi kuachana na imani za kishirikina na kuamini ramli chonganishi zinazosababisha madhara kwa watu wasio na hatia.

spot_img

Latest articles

Sangweni: Sekta ya Mafuta na Gesi Ni Chachu ya Ukuaji wa Uchumi wa Taifa

Na Mwandishi Wetu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli...

VETA Kihonda yaja ‘cold room’ kupunguza upotevu wa mazao ya wakulima

Na Mwandishi Wetu UBUNIFU wa mfumo jumuishi wa kuhifadhi mazao kwa kutumia teknolojia ya ubaridi...

Ofisi ya Msajili wa Hazina yalenga kukusanya Sh2 trilioni mwaka 2026/27

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imejiwekea lengo la kukusanya Sh2...

MAULIDI KITENGE AUNGANA NA TANESCO KUHAMASISHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA KWA UMEME

📌 Aahidi kutumia jukwaa lake kuhamasisha wananchi kutumia umeme kwa shughuli za kupikia 📌 Ushirikiano...

More like this