COASCO: Ukaguzi wa vyama vya ushirika waongeza uwazi na kuimarisha imani ya wanachama

Na Tatu Mohamed

Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO) limesema ukaguzi unaofanywa katika vyama vya ushirika umeendelea kuongeza uwazi, uwajibikaji na kuimarisha imani ya wanachama katika uendeshaji wa vyama hivyo nchini.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COASCO, CPA Jeremiah Mugeta, alisema hayo alipotembelea banda la Wizara ya Kilimo katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), ambapo taasisi mbalimbali zilizo chini ya wizara hiyo zinaonesha huduma na shughuli zinazotekelezwa katika kuendeleza sekta ya kilimo.

Alisema ushirika una nafasi kubwa katika kukuza kilimo na uchumi wa taifa kwa kuwa unawaunganisha wakulima na kuwawezesha kufanya shughuli zao kwa pamoja, huku COASCO ikiwa na jukumu la kuhakikisha vyama hivyo vinaendeshwa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.

“Ukaguzi ni muhimu kwa sababu unatoa picha halisi ya mwenendo wa vyama vya ushirika, matumizi ya fedha na kusaidia kutoa ushauri wa namna ya kuimarisha utendaji wa vyama hivyo,” alisema Mugeta.

Alieleza kuwa COASCO imejipanga kuhakikisha vyama vyote vya ushirika vinapata huduma za ukaguzi na ushauri ili viweze kuimarika zaidi na kutoa manufaa kwa wanachama wake.

Amesema katika mwaka wa fedha 2026/2027, shirika hilo litaendelea na mpango wa kufanya ukaguzi wa vyama vya ushirika nchini, huku akiwataka viongozi wa vyama hivyo kuandaa taarifa za fedha kwa wakati ili kurahisisha mchakato wa ukaguzi.

Kwa mujibu wa Mugeta, hali ya uendeshaji wa vyama vya ushirika imeendelea kuimarika ikilinganishwa na miaka iliyopita, ambapo idadi ya vyama vinavyopata hati safi imeongezeka kutoka asilimia nne hadi zaidi ya asilimia 16.

Alisema mafanikio hayo yanaonesha kuwa jitihada za Serikali katika kuimarisha sekta ya ushirika zimeanza kuleta matokeo chanya.

Aidha, Mugeta alisema sekta ya kilimo ina mchango mkubwa katika uchumi wa Tanzania, ikichangia zaidi ya asilimia 26 ya pato la taifa, huku ushirika ukiwa sehemu muhimu ya kuongeza thamani ya mazao na kukuza kipato cha wakulima.

Aliwahimiza wanachama wa vyama vya ushirika kushirikiana na wakaguzi na kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu za uendeshaji ili kuendelea kujenga vyama imara na vyenye tija.

COASCO imeendelea kusisitiza kuwa kupitia ukaguzi na utoaji wa ushauri wa kitaalamu, vyama vya ushirika vitaendelea kuwa nguzo muhimu katika maendeleo ya kilimo na uchumi wa Tanzania.

spot_img

Latest articles

JAB yazindua mwongozo wa kisheria wa utoaji wa Ithibati ya maisha kwa waandishi

Na Mwandishi Wetu BODI ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imezindua rasmi Mwongozo wa...

BRELA YAIBUA FURSA MPYA ULINZI WA ALAMA ZA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI

Na Mwandishi Wetu Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewataka wajasiriamali wanaoshiriki...

TTB yakutanisha wadau kujadili mustakabali wa Destination Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya...

Dkt. Jafar Seif: Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Sabasaba larahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za...

More like this

JAB yazindua mwongozo wa kisheria wa utoaji wa Ithibati ya maisha kwa waandishi

Na Mwandishi Wetu BODI ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imezindua rasmi Mwongozo wa...

BRELA YAIBUA FURSA MPYA ULINZI WA ALAMA ZA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI

Na Mwandishi Wetu Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewataka wajasiriamali wanaoshiriki...

TTB yakutanisha wadau kujadili mustakabali wa Destination Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya...