TPRB YAENDELEA KUTOA HUDUMA SABASABA, YAPOKEA MAOMBI YA USAJILI

Na Mwandishi Wetu

Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB) imeendelea kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi na wadau katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Katika banda la TPRB lililopo ndani ya Banda la Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bodi imejikita katika kupokea na kushughulikia maombi ya usajili kutoka kwa wataalamu wa mipangomiji wanaotembelea banda hilo.

Maafisa wa TPRB wanatoa huduma ana kwa ana kwa waombaji, ikiwa ni pamoja na kupokea nyaraka za usajili, kutoa maelekezo ya taratibu husika, na kusaidia kuhakikisha maombi yanawasilishwa kwa usahihi na kwa wakati.

Awali akizungumza katika maonesho hayo, Kaimu Msajili wa TPRB, TP. Martha Mkupasi, alisema kuwa ushiriki wa Bodi katika Sabasaba unalenga kuwafikia wadau wengi zaidi na kurahisisha huduma za usajili kwa vitendo.

Alisema kuwa Bodi inaendwlea kutoa elimu ya shughuli za mipangomiji kwa wananchi, ushauri pamoja na kupokea kero mbalimbali zinazohusiana na Bodi hiyo.

Katika muendelezo wa maonesho hayo, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Leonard Akwilapo, alitembelea banda la TPRB na kuipongeza Bodi kwa juhudi zake za kuboresha huduma na kuwasogezea wananchi huduma muhimu.

Aidha, Waziri huyo amesisitiza umuhimu wa Bodi kuendelea kutoa elimu kwa wananchi na kutoa huduma bora.

Pia, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bi. Lucy Kabyemela, alitembelea banda hilo na kujionea huduma zinazotolewa pamoja na kupongeza jitihada za Bodi katika kusogeza huduma karibu na wananchi.

TPRB inashiriki maonesho hayo, yaliyoanza rasmi Juni 28 na yanatarajiwa kuhitimishwa Julai 13, 2026 jijini Dar es Salaam.

spot_img

Latest articles

JAB yazindua mwongozo wa kisheria wa utoaji wa Ithibati ya maisha kwa waandishi

Na Mwandishi Wetu BODI ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) imezindua rasmi Mwongozo wa...

BRELA YAIBUA FURSA MPYA ULINZI WA ALAMA ZA BIASHARA KWA WAJASIRIAMALI

Na Mwandishi Wetu Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) imewataka wajasiriamali wanaoshiriki...

TTB yakutanisha wadau kujadili mustakabali wa Destination Tanzania

Na Mwandishi Wetu Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya...

Dkt. Jafar Seif: Banda la Ofisi ya Waziri Mkuu Sabasaba larahisisha upatikanaji wa huduma kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu NAIBU Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu – Tawala za...

More like this