EWURA CCC yatoa elimu ya matumizi sahihi ya nishati na maji Sabasaba

Na Mwandishi Wetu

BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA CCC) linaendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi sahihi ya huduma za maji, umeme, mafuta na gesi katika Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba), likilenga kuwajengea uelewa wa haki na wajibu wao kama watumiaji wa huduma hizo.

Afisa Uelimishaji na Uhamasishaji Mwandamizi wa EWURA CCC, Lugiko Lugiko, alisema maonesho hayo yamekuwa fursa muhimu ya kuwafikia wananchi moja kwa moja na kuwapa maarifa yatakayowasaidia kutumia huduma za nishati na maji kwa usalama na ufanisi.

Alisema elimu hiyo pia inalenga kuwasaidia wananchi kupunguza matumizi yasiyo ya lazima, kuepuka bili kubwa zinazotokana na matumizi yasiyo sahihi na kujua hatua za kuchukua wanapokutana na changamoto katika huduma wanazopokea.

“Tunataka wananchi wawe na taarifa sahihi kuhusu huduma wanazotumia. Mtumiaji anayefahamu haki na wajibu wake ana uwezo wa kufanya maamuzi sahihi na kulinda maslahi yake,” alisema Lugiko.

Alieleza kuwa kwa watumiaji wa umeme, EWURA CCC inasisitiza umuhimu wa kutumia mafundi wenye leseni, kufunga vifaa vinavyokidhi viwango vya ubora na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara wa mfumo wa umeme ili kupunguza matumizi makubwa ya nishati na kuzuia ajali.

Kuhusu huduma za maji, Lugiko aliwataka wananchi kufuatilia usomaji wa mita zao na kuhakikisha hakuna uvujaji wa maji katika mifumo yao, akisema baadhi ya bili kubwa husababishwa na hitilafu zinazoweza kuzuilika.

Aidha, aliwahimiza watumiaji wa mafuta kuhakiki bei elekezi zinazotolewa na EWURA, kuhakikisha pampu inaanza kuhesabu kutoka sifuri kabla ya kujaza mafuta na kudai risiti kwa kila manunuzi wanayofanya.

Pia alisisitiza umuhimu wa kununua mafuta katika vituo vyenye leseni ili kujiepusha na bidhaa zisizo na ubora unaotakiwa.Kwa upande wa nishati safi ya kupikia, Lugiko alisema wananchi wanapaswa kuendelea kutumia umeme na gesi kwa kuwa ni salama, zinasaidia kulinda mazingira, kuboresha afya na kupunguza muda wa kupika.

Aliwahimiza wananchi kutembelea banda la EWURA CCC katika maonesho hayo ili kupata elimu zaidi kuhusu matumizi salama ya huduma za nishati na maji pamoja na njia za kulinda haki zao kama watumiaji.

spot_img

Latest articles

RAIS SAMIA AAGIZA WAKUU WA MIKOA KUJIANDAA NA UDHIBITI WA ATHARI ZA ELNINO

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

Rais Samia azindua Kituo cha kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

JNHPP kuongeza Umeme wa Gridi ya Taifa kwa asilimia 45

Na Tatu Mohamed BWAWA la Julius Nyerere (JNHPP) linatarajiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo...

Tanzania kuandika historia leo, Rais Samia kuzindua Bwawa la Julius Nyerere

Na Tatu Mohamed TANZANIA inaandika ukurasa mpya katika historia ya sekta ya nishati leo...

More like this