FCC yatoa elimu ya ulinzi wa mlaji na ushindani wa haki Sabasaba

Na Mwandishi Wetu

Tume ya Ushindani (FCC) imeendelea kutumia Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (Sabasaba) kuwaelimisha wananchi na wafanyabiashara kuhusu sheria za ushindani, ulinzi wa mlaji na namna ya kutambua bidhaa bandia, huku ikitoa huduma mbalimbali papo kwa papo.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Mahusiano kwa Umma wa FCC, Roberta Feruzi, alisema maonesho hayo yameipa tume fursa ya kusogeza huduma karibu na wananchi kwa kupokea na kushughulikia malalamiko, kutoa ushauri wa kisheria pamoja na huduma nyingine zinazotolewa na taasisi hiyo.

Alisema sehemu kubwa ya elimu inayotolewa inalenga kuwajengea wafanyabiashara uwezo wa kuendesha biashara kwa kuzingatia misingi ya ushindani wa haki, kulinda maslahi ya walaji na kuepuka vitendo vinavyokiuka sheria za ushindani.

“Tunataka wafanyabiashara na wananchi wafahamu haki na wajibu wao. Elimu hii inawasaidia kufanya biashara katika mazingira ya ushindani wa haki na kuwapa uwezo wa kutambua na kuripoti bidhaa bandia pamoja na vitendo vinavyowaumiza walaji,” alisema Feruzi.

Alibainisha kuwa tangu kuanza kwa maonesho hayo, FCC imewafikia zaidi ya wajasiriamali 700 kupitia semina na ziara katika mabanda mbalimbali, ambapo wamepatiwa elimu kuhusu ushindani wa biashara, ubunifu na fursa zinazotolewa na Serikali kwa sekta binafsi.

Kwa mujibu wa Feruzi, programu hiyo pia imewahusisha vijana wanaoanzisha biashara (startups), ambao wamehamasishwa kutembelea ofisi za FCC zilizopo Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Mwanza na Mbeya kwa ajili ya kupata ushauri na mwongozo wa kukuza biashara zao.

Alisisitiza kuwa utoaji wa elimu kwa umma utaendelea hata baada ya kumalizika kwa Maonesho ya Sabasaba, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa FCC wa kujenga mazingira ya biashara yenye ushindani wa haki na kulinda maslahi ya watumiaji nchini.

Aidha, aliwahimiza wananchi na wadau wa biashara kutembelea banda la Wizara ya Viwanda na Biashara ili kupata elimu na huduma zinazotolewa na FCC pamoja na taasisi nyingine zilizo chini ya wizara hiyo.

spot_img

Latest articles

RAIS SAMIA AAGIZA WAKUU WA MIKOA KUJIANDAA NA UDHIBITI WA ATHARI ZA ELNINO

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

Rais Samia azindua Kituo cha kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

JNHPP kuongeza Umeme wa Gridi ya Taifa kwa asilimia 45

Na Tatu Mohamed BWAWA la Julius Nyerere (JNHPP) linatarajiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo...

Tanzania kuandika historia leo, Rais Samia kuzindua Bwawa la Julius Nyerere

Na Tatu Mohamed TANZANIA inaandika ukurasa mpya katika historia ya sekta ya nishati leo...

More like this