Mbeya City yabaki Ligi Kuu,  kocha akiri kukumbana na changamoto

Na Mwandishi Wetu

Klabu ya Mbeya City imefanikiwa kusalia Ligi kuu ya soka  Tanzania bara kufuatia ushindi wa jumla wa 2-0 dhidi ya Tanzania Prisons kwenye michezo miwili ya mchujo (playoff) wa kusalia Ligi kuu.

Mbeya City iliibuka na ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza kabla ya kutoshana nguvu kwa sare tasa kwenye mchezo wa pili uliopigwa leo Julai 8,2026,  dimba la Sokoine, Mbeya huku Prisons wakielekea kwenye mchujo wa pili dhidi ya timu ya Polisi Tanzania kutoka Championship ili kujinusuru kushuka daraja.

 Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo, Kocha wa Mbeya City, Salim Mayanga amesema wamejifunza kutokana na changamoto walizokutana nazo na wanachosubiri ni mabadiliko kwa ajili ya msimu ujao.

 “Timu itafanya marekebisho kwenye maeneo yote yaliyokuwa na udhaifu mkubwa msimu huu. Kutakuwa na ulazima wa kuongeza wachezaji wenye uwezo kwenye maeneo ambayo yalionekana kuwa na mapungufu makubwa,” amesema Mayanga.

 Aidha Mayanga ametoa shukrani zake kwa mashabiki wa Mbeya na uongozi wa timu kwa ushirikiano wao, huku akiahidi kuwa wataendelea kufanya tathmini ya kina kuhusu kiwango cha ushindani wa ligi na jinsi ya kuleta mabadiliko chanya ndani ya kikosi hicho.

spot_img

Latest articles

RAIS SAMIA AAGIZA WAKUU WA MIKOA KUJIANDAA NA UDHIBITI WA ATHARI ZA ELNINO

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

Rais Samia azindua Kituo cha kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan,...

JNHPP kuongeza Umeme wa Gridi ya Taifa kwa asilimia 45

Na Tatu Mohamed BWAWA la Julius Nyerere (JNHPP) linatarajiwa kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezo...

Tanzania kuandika historia leo, Rais Samia kuzindua Bwawa la Julius Nyerere

Na Tatu Mohamed TANZANIA inaandika ukurasa mpya katika historia ya sekta ya nishati leo...

More like this