RAIS SAMIA AAGIZA WAKUU WA MIKOA KUJIANDAA NA UDHIBITI WA ATHARI ZA ELNINO

Na Mwandishi Wetu

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Taasisi mbalimbali za serikali kujiandaa mapema kukabiliana na mvua kubwa zinazotabiriwa nchini, ili kuepusha maafa na madhara kwa wananchi.

Rais Samia amesema taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) zinaeleza uwezekano wa kuwepo kwa mvua kubwa zinazohusishwa na hali ya El Niño, hivyo viongozi wanapaswa kuchukua hatua za tahadhari mapema.

“Niwaombe nendeni mkajitayarishe, mkaweke mazingira sawa ili mvua hizo zitakapoanza zisilete maafa makubwa kwa wananchi wetu,” amesema.

Amesema tahadhari ambazo TMA imeanza kutoa zinapaswa kuchukuliwa kwa uzito na viongozi kuhakikisha mazingira yanaandaliwa ili kupunguza athari zinazoweza kusababishwa na mvua hizo.

“Kwa hiyo niwaombe sana, tahadhari zimeanza kutolewa, hatua zichukuliwe ili mvua hizi zisilete madhara kwa wananchi wetu,” amesema Rais Samia.

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumamosi, Agosti 22, 2026, wakati akizungumza na wananchi Mkoani Pwani mara baada ya kuzindua Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Megawati 2,115 wa Bwawa la Mwalimu Julius Nyerere.

spot_img

Latest articles

TANESCO YABORESHA MAISHA YA WAFANYAKAZI NYUMBA YA MUNGU

📌 Nyumba za wafanyakazi zakarabatiwa, kuboresha utendaji wa kazi 📌 Mtambo wa kisasa wa kuchakata...

KATAMBI ATOA ONYO KWA MAKUNDI YA ULINZI YASIYO RASMI

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, ametoa onyo kwa...

Watumishi OTR wapatiwa mafunzo ya Mfumo wa Usimamizi wa Ubora

Na Mwandishi wa OTR OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) imeendelea na hatua za kuimarisha...

MRADI WA UMEME MPOMVU – GGM KUIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI GEITA – MHE. SALOME

📌 Kukamilika kwa njia mpya kutatoa fursa kwa njia ya awali kuendelea kunufaisha wananchi...

More like this