Ofisi ya Msajili Hazina yalenga kukusanya Sh1 trilioni kama mapato yasiyo ya kodi

Na Mwandishi Wetu

OFISI ya Msajili wa Hazina ina shauku ya kukusanya Sh1 trilioni kama mapato yasiyo ya kodi katika mwaka huu wa fedha wa 2024/25.

Akizungumza katika kikao na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam Jumatatu, Juni 2, 2025, Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu alisema tayari karibia Sh900 bilioni zimekusanywa kutoka taasisi za umma na kampuni ambazo serikali ina umiliki wa hisa chache zipatazo 200.

“Hadi kufikia sasa (Juni 2, 2025) Ofisi ya Msajili wa Hazina imekusanya karibia Sh900 bilioni kama mapato yasiyo ya kodi na matamanio yetu ni kukusanya Sh1 trilioni katika mwaka wa fedha wa 2024/25,” amesema Mchechu.

Amefafanua kuwa, ikiwa Ofisi hiyo itafanikiwa kukusanya Sh1 trilioni, itakuwa ni ongezeko la asilimia 30.4 ikilinganishwa na mwaka wa fedha uliopita ambapo kiasi cha Sh767 bilioni kilikusanywa.

Ili kuhakikisha Ofisi hiyo inafikia adhima hiyo ya kukusanya Sh1 trilioni, Msajili wa Hazina amezitaka taasisi ambazo bado hazijawasilisha gawio zifanye hivyo ndani ya wiki hii.

“Taasisi zote ambazo bado hazijawasilisha gawio kwa serikali, kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina, zinapaswa kufanya hivyo ndani ya wiki hii ili ifikapo siku ya Gawio, Juni 10 mwaka huu, asiwepo wa kudaiwa,” amesema Mchechu.

Mchechu amesema ukuaji wa mapato yasiyo ya kodi umetokana na kuimarishwa kwa utaratibu wa ufuatiliaji wa karibu wa gawio na michango katika Mashirika ya umma na matumizi ya Mifumo ya TEHAMA.

“Ofisi imefanikiwa kuunganisha Mfumo wa Mpango na Bajeti (PlanRep) na Mifumo ya ERMS na e-Watumishi pamoja na kufanya maboresho ya Mfumo wa MUSE ambao unawezesha kupata taarifa halisi za matumizi katika Taasisi na Mashirika ya Umma ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa fedha za Umma,” amesema Mchechu.

Amesema maboresho hayo sasa yamefanya mifumo kubadilishana taarifa ipasavyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Rais Samia Suluhu Hassan aliyetaka kuona mifumo inasomana.

spot_img

Latest articles

Tume Jaji Chande imekwepa kututajia aliyekutwa na ngozi ya ng’ombe

NINGALI ninaitafakari ripoti ya Jaji Mohammed Chande ya matukio ya Oktoba 2025 wakati na...

Adaiwa kumuua mtalaka wake kwa panga kisa nguvu za kiume

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi mkoani Lindi linamshikilia Hassan Athuman Mpogo (46), mvuvi na...

Rais Ruto kuhutubia Bunge Tanzania

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Kenya, William Ruto, anatarajiwa kuhutubia Bunge la Tanzania Mei 5,...

Mwigizaji, msanii wa Bongo Flava wafariki dunia

Na Mwandishi Wetu MSANII wa filamu nchini, Hashim Kambi, amefariki dunia leo alasiri akiwa anapatiwa...

More like this

Tume Jaji Chande imekwepa kututajia aliyekutwa na ngozi ya ng’ombe

NINGALI ninaitafakari ripoti ya Jaji Mohammed Chande ya matukio ya Oktoba 2025 wakati na...

Adaiwa kumuua mtalaka wake kwa panga kisa nguvu za kiume

Na Mwandishi Wetu JESHI la Polisi mkoani Lindi linamshikilia Hassan Athuman Mpogo (46), mvuvi na...

Rais Ruto kuhutubia Bunge Tanzania

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Kenya, William Ruto, anatarajiwa kuhutubia Bunge la Tanzania Mei 5,...