Mawaziri wa Nishati Jumuiya ya SADC kukutana nchini Zimbabwe

📌Masuala ya Umeme, Gesi, Nishati Safi kujadiliwa

Na Mwandishi Wetu

KAMISHNA wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga ameongoza jopo la Wataalam kutoka Wizara ya Nishati katika Kikao cha awali cha Kamati Ndogo ya Nishati ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), kilicholenga kujadili maandalizi ya Mkutano wa Pamoja wa Kamati ya Mawaziri wa SADC wanaoshughulikia masuala ya Nishati utakaofanyika nchini Zimbabwe.

Kikao hicho cha awali kimefanyika tarehe 30 Mei 2025 katika Ukumbi wa Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam kwa njia ya mtandao.

Mkutano wa Kamati ya Mawaziri wa SADC unatarajia kufanyika nchini Zimbabwe Mei 30 hadi Juni 04, 2025 ukitanguliwa na Mkutano wa Makatibu Wakuu wa Nishati wa SADC.

Kikao hicho cha Mawaziri kitajadili ajenda mbalimbali ikiwemo hali ya upatikanaji wa nishati ya umeme katika Kanda; Maendeleo ya sekta ndogo ya Mafuta na Gesi, Matumizi ya Nishati Safi na kujadili nafasi na utayari wa Kanda katika kutekeleza Azimo la Dar es Salaam lililotokana na Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika wa Misheni 300.

Washiriki wengine katika kikao hicho kilichofanyika kwa njia ya mtandao wametoka katika nchi zote zilizopo katika Jumuiya ya SADC.

spot_img

Latest articles

CRDB Foundation na GIZ wazindua mradi wa Ajira Ye2, kuzalisha zaidi ya ajira 500

Na Mwandishi Wetu TAASISI ya CRDB Bank Foundation kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la...

Taasisi za Umma zapitisha maazimio tisa ya kuimarisha ufanisi

Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma 650...

Chama aipa Singida Bs ubingwa wa CECAFA

Na Mwandishi Wetu Mabao mawili yaliyofungwa na Clatous Chama yamefanikisha timu ya Singida Bs kutwaa...

Makocha Yanga, Simba waanika kinachowapa jeuri

Na Winfrida Mtoi Kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii kesho Septemba 16,2025, makocha wa Simba...

More like this