Watanzania Watakiwa Kujitokeza Kuomba Nafasi 1,150 za Udereva Qatar

Na Mwandishi Wetu

WATANZANIA wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuchangamkia fursa ya ajira iliyotangazwa na Serikali kwa kushirikiana na Kampuni ya Al-MahaTravel and Tours ambapo nafasi 1,150 za kazi ya udereva wa mabasi ya mwendo kasi zinapatikana nchini Qatar.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Al-Maha Travel, Abdallah Mohamed, alisema mchakato wa usaili utaendeshwa kwa uwazi na hautamhusisha mwombaji kugharamia fedha yoyote, huku akiwahimiza madereva wenye vigezo kujitokeza kuomba nafasi hizo kwa wakati.

Alisema waombaji wanapaswa kuwa na leseni halali ya udereva Daraja C au E, umri kati ya miaka 25 hadi 50, hati halali ya kusafiria pamoja na uwezo wa kuwasiliana kwa lugha za Kiingereza au Kiarabu.

“Aidha, waombaji wote watatakiwa kuthibitisha afya zao kabla ya kuajiriwa. Watakaofanikiwa kuchaguliwa watalipwa mshahara wa Dola za Marekani 700 kwa mwezi pamoja na marupurupu mengine ikiwemo bima ya afya, chakula na malazi bila gharama,” alisema.

Vilevile, aliongeza kuwa gharama za tiketi ya ndege zitagharamiwa na mwajiri.

Alifafanua kuwa mwisho wa kupokea maombi ni Februari 04, 2026 na usaili utafanyika kuanzia Februari 6 hadi 8, 2026, ambapo madereva 900 wanahitajika kutoka Tanzania Bara na 250 kutoka Zanzibar.

spot_img

Latest articles

TCAA YAIMARISHA HUDUMA KWA WATEJA KUPITIA DAWATI MAALUM

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kupitia kwa Mkurugenzi wake...

VETA yajivunia ushindi, yaeleza mchango wa Mafunzo ya Ufundi Stadi

Na Mwandishi Wetu MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) imesema ushindi...

Twange: Tanesco yazidi kupanua Nishati Safi ya kupikia, kuimarisha usambazaji wa umeme Zanzibar

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Lazaro Twange, amesema Shirika...

WANANCHI WAENDELEA KUNUFAIKA NA OFA ZA TTCL SABASABA 2026

Na Mwandishi Wetu MAAFISA wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) wanaendelea kuwahudumia wananchi wanaotembelea...

More like this