Yanga yaingilia ugomvi wa Mangungu na mshabiki Simba

Na Mwandishi Wetu

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umesema umesikitishwa na kitendo cha vurugu alichofanyiwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu na mashabiki wa klabu hiyo jana Februari 1, 2025 baada ya mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ES Tunis ya Tunisia iliyochezwa kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa, Dar es Salaam.

Katika mchezo huo  ambao ilitoka sare ya mabao 2-2, licha ya kuongoza  kipindi chote cha kwanza ikienda mapumziko  ikiwa mbele kwa mabao 2-0, baadhi ya mashabiki walimvamia kiongozi huyo kwa kutaka kumpiga kutokana na kukasirishwa na matoke ohayo.

Akizungumza na waandishi wa habari, Ofisa Habari wa Yanga leo, Ally Kamwe, amesema vitendo vya aina hiyo, akiviita vya kihuni, havikubaliki katika michezo na vinachafua taswira ya soka la Tanzania.

“Tulishudia moja ya tukio la ovyo kwenye mchezo wa mpira wa miguu, moja ya tukio  la kishamba zaidi kufanyika hapa kwenye ardhi yetu, moja ya tukio la kihuni. Tukio hili lilimhususisha Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Murtaza Mangungu, video zikisambaa zikionesha akishambuliwa na mashabiki wa klabu hiyo.

“Yanga tunakemea na kupinga vikali vitendo vya kihuni vilivyofanyika,  lakini kama klabu tunapenda kumpa pole Mwenyekiti Mangungu na viongozi wote wa Simba waliokumbana na ghasia hiyo,” amesema Kamwe.

spot_img

Latest articles

Dk. Mwigulu ajadiliana na Kamati ya Maandalizi AFCON 2027

Na Mwandishi Wetu WAZIRI Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba amekutana na  Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi...

Coastal Union yawatembezea kichapo maafande wa Magereza

Na Mwandishi Wetu TIMU ya Coastal Union imetembeza kichapo cha mabao 4-1 kwa maafande wa...

Simba yazitaka pointi tatu kwa KMC kesho

Na Winfrida Mtoi KOCHA Mkuu wa timu ya Simba, Steve Barker ameweka wazi kuwa hakuna...

Msajili wa Hazina aikaribisha Jeune Afrique Media Group kuangazia fursa za uwekezaji

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na Frederic...

More like this