TFF yamfungia miaka sita Katibu Mkuu DRFA

Na Mwandishi Wetu

Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA),Ramadhan Missiru amefungiwa na Kamati ya Maadili ya Soka Tanzania (TFF), kutojihusisha na shughuli zozote za mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka sita ndani na nje ya nchi.

Kwa mujibu wa taarifa ya TFF iliyotolewa leo Mei 13, 2025 na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano, Clifford Ndimbo, Missiru alipatikana na hatia ya makosa mawili ya ukiukwaji wa maadili yaliyobainishwa na kamati hiyo katika kikao chake kilichofanyika Mei 8, 2025 jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo imesema kuwa Missiru alishtakiwa na Sekretarieti ya TFF kwa makosa mawili ikiwemo kushindwa kutii maamuzi ya Kamati ya Maadili, kinyume na Kanuni ya 73(8) ya Maadili ya TFF Toleo la 2021. Kosa lingine ni kuchochea umma, kinyume na Kanuni ya 73(4) ya Maadili ya TFF Toleo la 2021.

“Baada ya Kamati kusikiliza pande zote na kupitia nyaraka na vielelezo vilivyowasilishwa mbele yake. imemtia hatiani kwa makosa mawili na kumpa adhabu ya kumfungia  kijihusisha na masuala ya mpira wa miguu  ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha miaka sita na kulipa faini ya sh 5,000,000,”

Kwa upande wa Mkuu wa Idara ya Habari ya na Mawasiliano ya Klabu ya Azam, Thabit Zakaria ‘Zakazakazi’, aliyeshtakiwa katika kamati hiyo kwa kuchochea umma, kamati ilibaini hakuna ushahidi wa kutoasha kumtia hatiani.

spot_img

Latest articles

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...

Padre aliyepotea apatikana akiwa hai

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma limefanikiwa kumpata Padre Camillus Nikata wa Jimbo...

More like this

Rasmi Kocha Yanga afungashiwa virago usiku

Na Mwandishi Wetu Uongozi wa Klabu ya Yanga umevunja mkataba na Kocha Mkuu, Romain Folz. ...

Mwanamke ashikiliwa  Polisi kwa  kumuua mume wake na kumfukia ndani ya nyumba yao

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita linamshikilia mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina...