‘Makomandoo’ wazitia hasara Simba na Yanga

Na Mwandishi Wetu

KLABU za Simba na Yanga zimetozwa faini ta sh.5,000,000 kila moja kwa kosa la walinzi wake kugombana na kutoleana lugha za matusi wakati wa mchezo wa Dabi ya Kariakoo ulipigwa Machi 1,2026 kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Adhabu hiyo imetolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kwa mujibu wa kanuni ya 47:1 ya Ligi Kuu kuhusu udhibiti wa klabu.

Taarifa iliyotolewa na Bodi ya Ligi, Simba italazimika kulipa gharama za matengenezo ya mlango wa kuingilia chumba cha kufanyia mikutano ya wanahabari ambao walinzi wake walivunja ili kulazimisha  timu hiyo kuingia kwa kutumia chumba hicho  kwa ajili ya kuvalia kabla ya mchezo.

Pia mchezaji wa Simba David Kameta ametozwa faini y ash 1,000,000 kwa kosa la kuonekana akimwaga kimiminika kiwanjani dakika chache baada ya kuwasili uwanja wa Amaan kitendo kilichotafsiliwa kwa Imani za kishirikina.

Aidha Simba imetoza faini ya  jumla ya sh 10, 000,000 kwa makosa ya  kukataa kutumia chumba rasmi cha kuvalia na kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi ambapo kila kosa imetozwa sh, 5, 000,000.

spot_img

Latest articles

Rais Samia akabidhi 94.1 bilioni mikopo ya wanawake, vijana

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imekabidhi hundi ya shilingi 94.1 bilioni kwa ajili ya mikopo ya...

Mganga tiba za asili jela miaka 30 kwa kubaka

Na Mwandishi Wetu Mahakama ya Wilaya ya Kasulu imemhukumu mshitakiwa Nuru Hamimu Omary (48), mkulima...

DAWASA yawaunganishiwa maji kwa mkopo wakazi wa Kibosha

Na Mwandishi Wetu Wakazi zaidi ya 100 wa Kitongoji cha Kibosha Mji Mpya wamejitokeza kuomba...

Tume uchunguzi wa matukio Oktoba 29 kukabidhi ripoti, watu 63,603 watoa maoni

Na Mwandishi Wetu TUME ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na...

More like this