Trump: Sina uhakika na uwepo wa amani Israel na Hamas

Rais wa Marekani, Donald Trump amesema hana uhakika na kuwepo kwa amani ya kudumu kati ya Israel na Hamas licha ya kuwa sehemu ya mpango wa kusitisha mapigano uliowezesha kuachiwa kwa mateka ambapo akizungumza kabla ya mkutano wake na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, Trump amekiri kuwa hali bado ni tete na haitabiriki.

Netanyahu aliyewasili Washington kwa mazungumzo hayo anakabiliwa na shinikizo kali kutoka kwa washirika wake wenye msimamo mkali wa kisiasa ambao wanataka mashambulizi dhidi ya Hamas yaendelezwe lakini Wakati huo huo Wananchi wa Israel wanamtaka ahakikishe mateka waliosalia wanaachiwa na vita vya miezi 15 vinakoma.

Hata hivyo, Hamas imesisitiza kuwa haitatoa mateka zaidi bila Israel kuondoa Wanajeshi wake kutoka Gaza suala linalozua mgawanyiko ndani ya Serikali ya Netanyahu ambapo Bezalel Smotrich Mshirika wake wa siasa kali ametishia kuiangusha Serikali ikiwa vita dhidi ya Hamas havitaendelea.

Pamoja na hayo, Trump ameibua mpango wa kuwahamisha Wapalestina kutoka Gaza kwenda Misri na Jordan ingawa mataifa hayo yamekataa wazo hilo na Wachambuzi wanaonya kuwa msimamo huo wa Trump unaweza kuhatarisha juhudi za kufanikisha usuluhishi kati ya Israel na Saudi Arabia kwani mazungumzo hayo yanasisitiza kuwa suluhisho pekee ni kuundwa kwa Taifa huru la Palestina.

spot_img

Latest articles

Waziri wa Nishati Ndejembi azindua rasmi mita janja

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius Ndejembi amezindua rasmi mita janja (smart meter)...

RC Kunenge: Mto Ruvu ubaki kwa matumizi ya binadamu tu, tusitishe shughuli nyingine kwa muda

Na Mwandishi Wetu MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, ametoa wito kwa wakulima...

Tume ya Jaji Chande na mlima wenye utelezi

KAMA kuna tume ya uchunguzi iliyopata kuundwa nchini kwa jambo mahususi, ikajikuta katika uwanja...

Rais Samia: Walilenga kupindua dola

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa vurugu...

More like this