Tanzania yang’ara Tuzo za Utalii Duniani, yaingiza vipengele 41

Na Tatu Mohamed

TANZANIA imeendelea kung’ara katika anga la kimataifa baada ya kuingiza vipengele 41 katika Tuzo za Utalii na Usafirishaji Duniani (World Travel Awards), hatua inayoimarisha nafasi yake kama moja ya vinara wa utalii barani Afrika.

Akizungumza leo Aprili 11, 2026 jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Paulina Mkama, amesema tuzo hizo zinahusisha jumla ya washindani 85 kutoka sekta za umma na binafsi, zikilenga kutambua na kusherehekea ubora wa huduma, kuhamasisha ushindani na kutoa fursa kwa wadau na watalii kupigia kura vivutio bora duniani.

Paulina ameeleza kuwa ushiriki wa Tanzania katika tuzo hizo ni fursa adhimu ya kuitangaza nchi kimataifa na kuiweka katika ramani ya dunia kama kitovu cha utalii.

Ameongeza kuwa taasisi za serikali, ikiwemo TFS na TAWA, zimefanikiwa kuwasilisha vivutio vyake katika kinyang’anyiro hicho.

“Kwenye kinyang’anyiro hicho, Tanzania imewania nafasi katika vipengele mbalimbali barani Afrika, huku vivutio vikubwa kama Hifadhi ya Taifa ya Serengeti vikitajwa kuwania tuzo za juu.

“Aidha, katika baadhi ya vipengele, washindani saba kati ya 14 wanatoka Tanzania, hali inayoonesha uimara na ushindani wa sekta ya utalii nchini,” amesema.

Amebainisha kuwa sekta ya utalii inachangia zaidi ya ajira milioni moja kila mwaka, na mafanikio katika tuzo hizi yataongeza fursa za uwekezaji, ajira pamoja na kukuza pato la taifa.

“Kauli mbiu ya kampeni yetu ni “Kura Moja, Tiketi Moja kwa Tanzania” inaendelea hivyo tunawahamasisha Watanzania na wadau wa utalii kushiriki kikamilifu kupigia kura nchi ili kuongeza nafasi ya ushindi,” amesema.

Amefafanua kuwa, mbali na kuimarisha ushindani wa ubora wa huduma, tuzo hizo pia huchochea ukuaji wa sekta ya utalii kupitia ubunifu, uwekezaji na kuongeza mvuto wa vivutio katika soko la kimataifa.

“Kwa mara ya kwanza, baadhi ya vivutio vinavyosimamiwa na taasisi za serikali kama TAWA na TFS ikiwemo Mpanga Kipengere, Aman Forest Reserve, Selous Game Reserve, Pugu Kazimzumbwi na Kilwa Kisiwani, vimeingia kwenye ushindani huo, jambo linaloashiria kukua kwa sekta ya utalii nchini,” ameongeza.

spot_img

Latest articles

OTR na IMF zajadili utendaji wa taasisi za umma

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na ujumbe wa Shirika la Fedha...

MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU YAPUNGUA KUTOKA 98,754 HADI 33,511

Na Tatu Mohamed MAAMBUKIZI mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini yamepungua kutoka watu 98,754...

MRADI WA UPANUZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME DEGE KUIMARISHA HALI YA UPATIKANAJI WA UMEME KIGAMBONI

📌Wafikia Asilimia 90 katika utekelezaji wake 📌 Kukamilika Mwisho wa Mwezi Disemba 2026 Na Mwandishi Wetu...

GBT yaikaribisha BetSasa sokoni, yaitaka kuzingatia maadili

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), James Mbalwe ameikaribisha...

More like this

OTR na IMF zajadili utendaji wa taasisi za umma

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na ujumbe wa Shirika la Fedha...

MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU YAPUNGUA KUTOKA 98,754 HADI 33,511

Na Tatu Mohamed MAAMBUKIZI mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini yamepungua kutoka watu 98,754...

MRADI WA UPANUZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME DEGE KUIMARISHA HALI YA UPATIKANAJI WA UMEME KIGAMBONI

📌Wafikia Asilimia 90 katika utekelezaji wake 📌 Kukamilika Mwisho wa Mwezi Disemba 2026 Na Mwandishi Wetu...