MIILI YA WANAFUNZI WALIOFARIKI KWA RADI YAAGWA

Na Mwandishi Wetu

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe,  Dk. Doto Biteko ameongoza waombolezaji  kuaga miili ya wanafunzi saba wa Shule ya Sekondari Businda iliyopo wilayani Bukombe, Geita waliofariki kwa kupigwa na radi  Januari 27, 2025.

Katika shughuli ya kuaga miili hiyo iliyofanyika leo Januari 30,2025, Dk. Biteko amekabidhi ubani kwa wafiwa huku akiwataka kuwa wavumilivu hasa kipindi hiki cha majonzi.

Ametoa pole kwa wazazi, walezi ndugu wa watoto pamoja na wanafunzi wa Businda kwa kuondokewa na wapendwa wao na wanajamii wa Businda Sekondari kwa jitihada na utoaji wa huduma wakati wa tukio hilo.

“ Imeandikwa kwamba shukuruni Mungu kwa kila jambo, Mungu ametukutanisha leo katika hali ya majonzi. Tukio hili litukumbushe kutenda mema wakati wote na tuamini kwamba Mungu ndiye mwenye uweza. Kipekee ningetamani kuwataja Madaktari wote kwa majina kutokana na msaada mkubwa walioutoa lakini itoshe kusema asante kwa kazi kubwa mliyoifanya,” amesema Dk. Biteko.

Amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan baada ya kupokea taarifa za msiba huo mzito amekuwa akifuatilia kwa karibu na kutoa maelekezo kwa ajili ya kuzifariji familia za wafiwa, wana Bukombe na Taifa kufuatia kuondokewa na vijana waliokuwa katika safari ya kutafuta elimu.

“Rais Samia amegharamia msiba pamoja na kutoa ubani kwa kila familia za wafiwa pamoja na kugharamia usafirishaji wa miili ya wanafunzi wawili kwenda Chato, Geita na Karatu mkoani Arusha kwa mazishi,” amesema.

Naye Mkuu wa Shule ya Sekondari Bulangwa, Theodora Mushi amesema wanafunzi hao walipatwa na umauti wakiwa katika harakati za kusaka elimu.

Wanafunzi wanne kati yao walifariki papo hapo na wengine watatu walifariki wakati wakipatiwa matibabu katika hospitali na vituo mbalimbali vya afya.

spot_img

Latest articles

TANZANIA YAZIDI KUIMARISHA NAFASI YAKE KATIKA BIASHARA YA UMEME KIKANDA

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar TANZANIA imeendelea kuimarisha nafasi yake katika biashara ya umeme kikanda, huku...

MRADI WA NJIA YA KUSAFIRISHA UMEME WA KV 220 IGANJO–SAZA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME NA KUCHOCHEA UCHIMBAJI WA MADINI – MHE. SALOME

📌 Ashuhudia utiaji saini mkataba wa utekelezaji wa mradi kutoka Iganjo, Mbeya hadi Saza,...

Salome Ashuhudia utiaji saini mkataba wa sh. bilioni 198 kuimarisha umeme Songwe, Chunya

📌Ataka kasi ya utekelezaji wa mradi na wazawa kupewa kipaumbele 📌Wachimbaji wapongeza Na Mwandishi Wetu NAIBU...

ZARA TANZANIA ADVENTURES YAZINDUA RASMI KAMPENI YA TWENZETU KILELENI MSIMU WA TANO

KAMPUNI ya Zara Tanzania Adventures imezindua rasmi kampeni ya Twenzetu Kileleni – Msimu wa...

More like this