SACP Mahanga: Ulinzi viwanjani unahitaji ujasili

Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Polisi Jamii Kamisheni ya Polisi Zanzibar, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Jonas Mahanga amesema suala la ulinzi na usalama katika viwanja vya michezo linahitaji moyo na ujasiri pamoja na uadilifu ili kuweza kufikia malengo ya kuimarisha sekta za michezo.

Ameyasema hayo wakati wa kufunga mafunzo ya siku tatu ya maofisa wa ulinzi na usalama viwanjani, yaliyofanyika kwenye Uwanja wa New Amaan Complex ambayo yaliandaliwa na Shirikisho la Soka Zanzibar (ZFF).

Amesema siku zote katika kufikia mafanikio ni lazima kuwe na watu waliojitolea kwa hali na mali na wenye uchungu wa kutaka kufikia mafanikio husika.

Ameeleza kuwa kazi ambayo wameisomea ni ngumu katika mazingira yaliyowazunguka, hivyo inahitaji ujasiri wa hali ya juu na kuwa na uadilifu kwa maslahi ya michezo.

“Hii ni kazi ngumu wala musione masihara na ukiichukulia urahisi hatuwezi kufika mbali ni lazima tuwe makini na tuache muhali”, amesema SACP Mahanga.

Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo, Ramadhan Manyama amesema washiriki hao walipata mafunzo hayo kwa muda wa siku tatu na watakabidhiwa vyeti vya kuhitimu mafunzo hayo.

Amesema walijifunza mada mbalimbali kuhusiana na masuala ya ulinzi na anaamini wameyaelewa na watakuwa na mabadiliko viwanjani.

Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Zanzibar, Issa Kassim Ali amesema baada ya mafunzo hayo ana imani kuwa watashirikiana katika masuala yao mbalimbali viwanjani.

Naye Mkuu wa Operesheni na Mafunzo Mkoa wa Kusini Pemba, ASP Hassan Khamis Juma, amesema
elimu waliyoipata wataenda kuifanyia kazi na watakuwa mabalozi kwa wengine ambao hawajapata mafunzo hayo hasa kisiwani Pemba.

spot_img

Latest articles

Chondechonde Polisi msisababishe wananchi wakate tamaa

ALHAMISI iliyopita yaani Desemba 5, mwaka huu wa 2024 lilitokea tukio baya la kuhuzunisha...

Ufaransa yaipatia Tanzania Sh bilioni 323.4

Na Mwandishi Wetu Serikali ya Tanzania na Shirika la Maendeleo La Ufaransa (AFD) wamesaini mikataba...

TANZANIA YAWEKA REKODI MKUTANO WA WAHASIBU WAKUU AFRIKA

Na Mwandishi Wetu Tanzania imeweka rekodi ya Mkutano wa Pili wa Wahasibu Wakuu wa Serikali...

TANZANIA KUPAMBANA NA JANGWA

Na Mwandishi wetu Serikali imejipambanua katika kupambana na kuenea kwa jangwa, kurejesha ardhi iliyoharibiwa pamoja...

More like this