Rais Samia azitaka Halmashauri kutoa huduma bora kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu

Rais  Dk. Samia Suluhu Hassan, amezitaka Halmashauri kutumia ofisi mpya zinazojengwa katika maeneo yao, kuboresha maeneo ya kazi na kutoa huduma bora na kutakua kwa wananchi

Akizungumza leo Septemba 25,2024 wakati akizindua jengo la ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma, amesema ofisi hizo zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa.

“Madhumuni ya Serikali kujenga nyumba hizi ni kuleta mazingira mazuri kwa Maafisa wetu wanaofanya kazi ndani ya Halmashauri hizi, wito wangu ni kwamba ofisi hizi zitumike kuondoa kero za wananchi, pili Mkurugenzi Mtendaji na watumishi wote muweze kulitunza jengo hili kama lilivyo leo, kila tukija lionekane hivihivi,” amesema Rais Samia.

Ameeleza kuwa serikali imeendelea kupeleka fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo na kuboresha huduma za jamii, hivyo kuwataka watendaji kuweka nguvu katika kusimamia miradi ili yanayowakera wananchi yaondoke.

“Utumishi wetu mimi na nyinyi  kuhudumia wanachi, sisi ni watumishi wa wananchi na sio mabwana wa wananchi, sio watawala wa wananchi, sisi ni watumishi kwa wananchi, ndio maana Serikali inashusha fedha nyingi ili zifanyiwe kazi wananchi hawa waondoshewe shida zao,” amesisitiza.

spot_img

Latest articles

TANESCO YABAINI MATUKIO YA WIZI WA UMEME KINONDONI KASKAZINI

📌 Operesheni ya ukaguzi wa mita yabaini matumizi yasiyo halali ya umeme eneo la...

‘Uandishi wa kidijitali ndiyo mpango mzima’

Na Mwandishi Wetu Kampuni ya Media Brains ikishirikiana na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS)...

Msajili wa Hazina ateta na uongozi wa kampuni ya Barrick

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi...

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

More like this