Tanzania yajipanga matumizi ya nishati ya nyuklia

Na Mwandishi Wetu

Tanzania imeeleza mpango na utayari wake katika uendelezaji wa nishati ya nyuklia ikiwa ni moja ya vyanzo mbadala vya nishati safi ya umeme kwa maendeleo ya kiuchumi na ustawi wa jamii.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko wakati akiwasilisha Mpango wa Tanzania katika Mkutano wa Pili wa Masuala ya Nishati ya Nyuklia kati ya Marekani na nchi za Afrika (US-Africa Nuclear Energy Summit) unaoendelea Jijini Nairobi, nchini Kenya.

“Utayari wa Tanzania katika kuendeleza na kutumia nishati ya nyuklia unatiliwa mkazo katika Sera ya Nishati ya mwaka 2015, Sera ya Madini ya mwaka 2009, Mpango Kabambe wa Kuendeleza Sekta ya Umeme na Mkakati wa Nishati Jadidifu ambapo nyaraka zote hizi zinatambua umuhimu wa nyuklia kukidhi mahitaji ya nishati nchini.” Ameeleza Dk. Biteko

Katika mkutano huo unaojumuisha viongozi katika sekta ya nishati, watunga sera na wataalam kutoka nchi mbalimbali barani Afrika, Dk. Biteko amesema Tanzania iko tayari kuendeleza nishati ya nyuklia ikiwa ni moja ya vyanzo vitakavyoiwezesha nchi kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika na ambayo inakidhi viwango vya kimataifa katika uhifadhi wa mazingira.

Amesema chini ya uongozi wa Rais, Dk. Samia Suluhu Hassan, Serikali inaendelea kuchukua hatua muhimu zitakazowezesha matumizi ya nishati nyuklia kama moja ya vyanzo vya nishati safi ambapo hadi sasa Tanzania ina mashapo ya madini ya urani takriban tani 58,500 ambayo yanaweza kutumika kama chanzo cha uzalishaji wa nishati ya nyuklia.

spot_img

Latest articles

Safari ya ‘TLP’ ya Lissu ni ipi?

MWAKA 1992 wakati nchi hii ilipoingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, kulikuwa...

Karibu 2025, tuyakatae magenge haya sasa

LEO ni siku ya pili katika mwaka mpya wa 2025. Ninawatakia wasomaji wa safu...

Kuubeba uozo wa 2024  kuingia 2025 ni fedheha

NI siku nne tu zimebakia kuupa kisogo mwaka 2024. Mwaka huu ulikuwa na mambo...

Hivi vikosi kazi vimerejea kwa mlango wa nyuma?

KUNA kila dalili kwamba taifa letu kidogokidogo linakumbwa na hali ya kutokuaminiana. Hali hii...

More like this

Safari ya ‘TLP’ ya Lissu ni ipi?

MWAKA 1992 wakati nchi hii ilipoingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, kulikuwa...

Karibu 2025, tuyakatae magenge haya sasa

LEO ni siku ya pili katika mwaka mpya wa 2025. Ninawatakia wasomaji wa safu...

Kuubeba uozo wa 2024  kuingia 2025 ni fedheha

NI siku nne tu zimebakia kuupa kisogo mwaka 2024. Mwaka huu ulikuwa na mambo...