‘Waandishi wa habari wasipokuwa makini nafasi yao itapotea katika jamii’

Mtandao wa Utetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) umewataka waandishi kujiandaa kuripoti habari za uchaguzi wa mwaka 2024 na 2025 ili kuwapa wananchi fursa ya kuchagua viongozi wanaofaa.

Akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari yanayoendelea mjini Dodoma Agosti 23, 2024, Mratibu wa THRDC Onesmo Olengurumwa, aliwakumbusha kwamba ni wajibu wao kutoegema upande wowote wa wagombea ili kuwapa wananchi taarifa sahihi kuhusu uchaguzi.

Alionya kwamba kama waandishi wataendelea kujiweka kando au kuegemea upande wowote, kama ambavyo wamezipa mgongo habari za mgogoro wa Ngorongoro, hakika wananchi wataendelea kulishwa taarifa na uandishi wa kijamii (citizen journalism) hivyo umuhimu wa waandishi kupotea.

Alisema kwamba ingawa kwa zaidi ya siku nne jamii inayoishi Ngorongoro imekuwa kwenye kampeni ya kudai haki yao huku vyombo vya habari vikijitenga nao, bado taarifa zao zimeendelea kutoka kwa sababu katika dunia ya sasa hakuna mtu mwenye uwezo wa kuzima tena habari zisitoke.

“Taarifa na picha mnazoziona kutoka Ngorongoro hata kama hakuna chombo cha habari pale, hata kama waandishi wamesusia, bado kwa kutumia simu za mkononi jamii ile imefanikiwa kutoa taarifa ya kinachoendelea,” alisema Olengurumwa.

Mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo waandishi ili watekeleze wajibu wao wa kuripoti chaguzi zinazokuja kwa weledi.

spot_img

Latest articles

Safari ya ‘TLP’ ya Lissu ni ipi?

MWAKA 1992 wakati nchi hii ilipoingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, kulikuwa...

Karibu 2025, tuyakatae magenge haya sasa

LEO ni siku ya pili katika mwaka mpya wa 2025. Ninawatakia wasomaji wa safu...

Kuubeba uozo wa 2024  kuingia 2025 ni fedheha

NI siku nne tu zimebakia kuupa kisogo mwaka 2024. Mwaka huu ulikuwa na mambo...

Hivi vikosi kazi vimerejea kwa mlango wa nyuma?

KUNA kila dalili kwamba taifa letu kidogokidogo linakumbwa na hali ya kutokuaminiana. Hali hii...

More like this

Safari ya ‘TLP’ ya Lissu ni ipi?

MWAKA 1992 wakati nchi hii ilipoingia katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, kulikuwa...

Karibu 2025, tuyakatae magenge haya sasa

LEO ni siku ya pili katika mwaka mpya wa 2025. Ninawatakia wasomaji wa safu...

Kuubeba uozo wa 2024  kuingia 2025 ni fedheha

NI siku nne tu zimebakia kuupa kisogo mwaka 2024. Mwaka huu ulikuwa na mambo...