Esther Bulaya: Nilikuwa Chadema kwa mkopo nimerejea, CCM ni kama  Barcelona 

Na Mwandishi Wetu

Aliyekuwa Mbunge wa viti maalumu kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Esther Bulaya  amesema  alikuwa Chadema kwa mkopo sasa amerejea  Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambacho ni sawa Barcelona  au Real Madrid na wanakwenda kutengeneza kikosi cha kushinda ‘Champions League’.

Bulaya   ambaye  amerejea  CCM na kuchukua fomu ya kugombea Ubunge, Jimbo la Bunda Mjini mkoani Mara kupitia CCM, amejinasibu  mbele ya waandishi wa habari kuwa  chama alichokuwepo ni kama timu iliyoshuka daraja, hivyo amerudi kutoka kwenye mkopo.

“Unapozngumzia Chama Cha Mapinduzi  ndio Barcelona ya Tanzania, Chama Cha Mapinduzi  kimerudisha usajili kwa wachezaji wake wa Barcelona ambao waliwatuma kwa mkopo kwenye timu ya Leicester City  ambayo imeshuka daraja,” amesema Bulaya.

Ameeleza kuwa alianza  harakati  ndani ya CCM tangu akiwa  vyuoni, hivyo  ana furaha kurejea katika chama kilichomlea.

Bulaya ni miongoni mwa wabunge 19 wa Viti Maalumu wa CHADEMA ambao chama hicho kilitangaza kuwavua uanachama, lakini walisalia bungeni hadi kuhitimishwa kwa Bunge la 12 kwa amri ya mahakama.

spot_img

Latest articles

Taasisi za Umma Kukabidhi gawio Ikulu Juni 30 Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina imetangaza siku ya Gawio 2026 itafanyika...

DC Mbarali aongoza zoezi la upandaji miti kuhifadhi mazingira ya mradi wa TAZA

📌 Lengo ni kuimarisha na kuhifadhi mazingira 📌 Maeneo yenye vyanzo vya maji vinavyochangia uzalishaji...

Wachezaji volleyball nchini watakiwa kujituma kuwavutia mawakala wa kimataifa

Na Mwandishi Wetu WACHEZAJI wa mpira wa wavu 'volleyball' wanaoshiriki Ligi ya Mkoa wa Dar...

More like this