DAWASA yaanza kufunga Pampu zitakazoimarisha huduma ya Maji

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA), imeanza rasmi zoezi la kufunga Pampu 3 kati ya Pampu 7 zilizowasili mapema Mwezi Mei Mwaka huu zinazotarajia kuimarisha na kupunguza changamoto za kihuduma katika Mikoa ya Dar es salaam na Pwani.

Pampu hizo zitakazofungwa katika Mitambo mikubwa ya uzalishaji Maji ya Ruvu Juu na Ruvu Chini zina thaman ya Shilingi Bilioni 16.5 na zimeanza kufungwa kwa awamu kwa kuanzia katika Mtambo wa Ruvu Juu ulioko eneo la Mlandizi Mkoani Pwani.

Akizungumzia zoezi la ufungaji wa Pampu hizo unaoendelea, Meneja wa Mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Juu, Mhandisi Juma Kasekwa amesema jumla ya Pampu tatu mpya zitafungwa mtamboni hapo na tayari wataalamu kutoka China wamefika ili kuhakikisha usimamizi sahihi wa ufungaji pampu hizo.

“Pampu zilizofika ni mahususi kwa kuchota maji ghafi kutoka mtoni na kuyasukuma katika mtambo wa kuyachakata/kusafisha maji, huku kuanza kufunga Pampu hizi ni ishara kubwa kwa Mamlaka kuwa sasa tunaenda kupunguza changamoto za kihuduma na kuimarisha huduma kwa kiwango kikubwa, Pampu hizi zitapunguza muda mwingi uliotumika zamani katika matengenezo ya Pampu za awali na zilizochangia kuwakosesha Wananchi huduma,” amesema Mhandisi Kasekwa.

spot_img

Latest articles

OTR na IMF zajadili utendaji wa taasisi za umma

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na ujumbe wa Shirika la Fedha...

MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU YAPUNGUA KUTOKA 98,754 HADI 33,511

Na Tatu Mohamed MAAMBUKIZI mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini yamepungua kutoka watu 98,754...

MRADI WA UPANUZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME DEGE KUIMARISHA HALI YA UPATIKANAJI WA UMEME KIGAMBONI

📌Wafikia Asilimia 90 katika utekelezaji wake 📌 Kukamilika Mwisho wa Mwezi Disemba 2026 Na Mwandishi Wetu...

GBT yaikaribisha BetSasa sokoni, yaitaka kuzingatia maadili

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), James Mbalwe ameikaribisha...

More like this