DAWASA yafafanua sababu ya ukosefu wa maji maeneo ya Kibaha hadi Kisarawe

Na Mwandishi Wetu

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetoa ufafanuzi kuhusu changamoto ya ukosefu wa huduma ya maji iliyowakumba wakazi wa maeneo yanayohudumiwa na Mtambo wa Uzalishaji Maji wa Ruvu Juu kuwa ni matengenezo makubwa yaliyolenga kuboresha na kuimarisha huduma zaidi.‎‎

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano DAWASA, Bi. Everlasting Lyaro, amesema kukosekana kwa huduma hiyo tangu Machi 26,2026 kulitokana na utekelezaji wa kazi muhimu tatu katika mtambo huo, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa uzalishaji na usambazaji wa maji kwa wananchi.

‎‎Bi. Lyaro amesema kazi zilizofanyika na zilizosababisha kuzimwa kwa Mtambo wa Ruvu Juu ni pamoja na ukarabati wa bomba kubwa la inchi 48 linalosafirisha maji ghafi kutoka chanzo cha Mto Ruvu kwenda mtamboni, Usafishaji wa mabeseni ya kuchuja tope sambamba na zoezi la kufunga pampu mpya tatu.‎‎

“Tayari kazi ya kudhibiti uvujaji wa maji katika bomba la inchi 48 imekamilika, na tunatarajia huduma ya maji kwa wananchi wanaohudumiwa na mtambo huu kuanza kurejea taratibu kuanzia usiku wa leo Machi 27 kwa sehemu kubwa.

“Mamlaka inaomba radhi kwa changamoto iliyojitokeza,” amesema Bi. Lyaro.

‎Aidha, DAWASA imeeleza kuwa katika kuimarisha uhakika wa huduma ya Maji tayari Pampu nne za Maji zimewasili kati ya Pampu nane ambapo pampu tatu zimeanza kufungwa katika Mtambo wa Ruvu Juu na pampu moja katika Mtambo wa Ruvu Chini uliopo Wilaya ya Bagamoyo.

‎‎Lyaro amebainisha kuwa ujio wa Pampu hizi ni ishara ya nia thabiti ya Serikali ya awamu ya Sita ya kuboresha na kuimarisha upatikanaji wa Maji kwa Wananchi wake ndani ya eneo la kihuduma la DAWASA‎

spot_img

Latest articles

TUNATAMANI KUWA MABALOZI WA VIPIMO – WANAFUNZI MWANZA

Na WMA - Mwanza WANAFUNZI kutoka shule mbalimbali za Msingi na Sekondari jijini Mwanza wameomba...

Msajili wa Hazina ataka mageuzi makubwa TBC

Na Mwandishi wa OTR MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, ametaka kufanyika kwa mageuzi makubwa...

CRDB YAZINDUA UGHAIBUNI LOAN KUSAIDIA WATANZANIA WALIOPATA AJIRA NJE YA NCHI

Na Mwandishi Wetu BENKI ya CRDB imezindua rasmi huduma ya mkopo ya Ughaibuni yenye...

Ofisi ya Msajili wa Hazina kuimarisha ushirikiano na taasisi za umma za China

Na Mwandishi Wetu OFISI ya Msajili wa Hazina (OTR) iko katika hatua za mwisho za...

More like this