Mabadiliko ya sheria ya sukari yatawakomboa Watanzania-SBT

Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Tanzania, Profesa Kenneth Bengesi, akizungumza na Wahariri na Waandishi wa Habari.

Na Mwandishi Wetu, Media Brains

Kufuatia upotoshaji unaoendelea kutolewa na baadhi ya watu wasiokuwa na ufahamu juu ya sheria mpya ya sukari, Bodi ya Sukari Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu mabadiliko hayo.

Bodi imeeleza kuwa sheria hiyo mpya, iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inalenga kudhibiti mfumuko wa bei ya sukari ili isimuumize mwananchi, kuhakikisha upatikanaji wa uhakika, uwazi katika usambazaji wake, pamoja na ufanisi kwenye viwanda vya sukari nchini.

Hayo yamesemwa Julai 5, 2024, na Mkurugenzi wa Bodi ya Sukari Tanzania, Profesa Kenneth Bengesi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Ufafanuzi huo umekuja baada ya baadhi ya wadau wa sekta ya sukari kuelezea sakata hilo bila kuwa na taarifa za kutosha, hali iliyoibua sintofahamu kwenye sekta hiyo nyeti nchini.

“Baadhi ya watu wanaoelezea suala la sukari hawana taarifa za kutosha, hivyo ni jukumu letu kama Bodi kutoa picha kamili ya namna gani Watanzania watafaidika na mabadiliko haya katika sheria ya sukari,” amesema Profesa Bengesi.

Profesa Bengesi ameendelea kufafanua kuwa baadhi ya hoja zilizofafanuliwa na Bodi ya Sukari Tanzania ni pamoja na uhaba wa sukari, malalamiko ya utoaji wa vibali, na mbinu zinazotumika kuhakikisha uhaba wa sukari nchini unaisha.

“Serikali imefanya mabadiliko haya kwa nia ya kuleta ahueni kwa wananchi na kuleta ufanisi katika sekta ya sukari. Tunawahakikishia wananchi kuwa mabadiliko haya yatasaidia kupunguza changamoto zilizopo na kuleta maendeleo endelevu katika sekta hii muhimu,” ameongeza Profesa Bengesi.

Kwa mujibu wa Profesa Bengesi, Bodi ya Sukari Tanzania itaendelea kutoa elimu kwa umma kuhusu sheria mpya ya sukari na mafanikio yanayotarajiwa kutokana na utekelezaji wake. Amewataka wananchi na wadau wa sekta ya sukari kuwa na subira na kuunga mkono juhudi za serikali katika kuboresha sekta hiyo.

spot_img

Latest articles

Jaji Mkuu Masaju amepita mlemle

JAJI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, George Mcheche Masaju amemaliza mwezi mmoja...

Ally Kamwe akiri kuvutiwa na Tshabalala

Na Mwandishi Wetu Ofisa Habari wa klabu  ya Yanga Ally  Kamwe amesema licha ya kuwa yupo upande...

Rais Mwinyi afungua Jengo Jipya la Tume ya Uchaguzi Zanzibar

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein...

Gwajima: Sitanyamaza watu wakiendelea kutekwa, tuwape Chadema ‘Reform’ ili Taifa lisonge mbele

Na Mwandishi Wetu MBUNGE wa Kawe anayemaliza muda wake na Askofu wa Kanisa la...

More like this

Jaji Mkuu Masaju amepita mlemle

JAJI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, George Mcheche Masaju amemaliza mwezi mmoja...

Ally Kamwe akiri kuvutiwa na Tshabalala

Na Mwandishi Wetu Ofisa Habari wa klabu  ya Yanga Ally  Kamwe amesema licha ya kuwa yupo upande...

Rais Mwinyi afungua Jengo Jipya la Tume ya Uchaguzi Zanzibar

Na Mwandishi Wetu RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein...