Ally Kamwe akiri kuvutiwa na Tshabalala

Na Mwandishi Wetu

Ofisa Habari wa klabu  ya Yanga Ally  Kamwe amesema licha ya kuwa yupo upande mwingine lakini  ni shabiki mkubwa wa wachezaji  wa Simba, Mohammed Hussein ‘Tshabalala na Shomari Kapombe kutokana na  uwezo mkubwa wa nyota hao.

Kamwe ametoa kauli hiyo kipindi ambacho kuna  na tetesi kuwa Yanga wanaitaka saini ya Tshabalala  katika kuimarisha kikosi chao.

“Nchi hii hapa  hakuna mwanadamu anaweza akadharau uwezo wa Mohamed Hussein Zimbwe na Shomari Kapombe, Mimi mwenyewe ni shabiki mkubwa wa hao watu wawili ni wachezaji wazuri,” amesema Kamwe.

Hata hivyo Kamwe hajaweka wazi kuwa klabu hiyo inamhitaji mchezaji huyo baada ya kusema bado hawajaanza usajili wala kutoa orodha ya wachezaji wanaoondoka klabuni hapo.

“Kuanzia tarehe 20 mwezi huu ndiyo  Yanga tutaanza kutoa taarifa rasmi ya nani katoka nani kaingia, sisi hatuna mambo ya ‘Thank You’ kipindi hiki,” amesema Kamwe.

spot_img

Latest articles

NDEJEMBI ASHUHUDIA UTIAJI SAINI WA MKATABA WA SHILINGI BILIONI 204.7 WA MRADI WA UMEME WA JUA WA MEGAWATI 100 KISHAPU

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Nishati, Deogratius J. Ndejembi, leo Julai 27, 2026, ameshuhudia...

DHAHABU YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 1.2 YAKAMATWA IKITOROSHWA

Na Mwandishi Wetu KUFUATIA kuimarishwa kwa mfumo wa udhibiti wa biashara haramu ya madini...

Taasisi za Umma zatakiwa kutokuwa kikwazo kwa wawekezaji

Na Mwandishi Pwani SERIKALI imezitaka Taasisi za Umma kuhakikisha zinakuwa chachu ya ukuaji wa uchumi...

SAMIA AONGOZA TAIFA KUWAKUMBUKA MASHUJAA WALIOJITOA KWA AJILI YA TANZANIA

Na Mwandishi Wetu MAMIA ya wananchi, viongozi wa Serikali na wakuu wa vyombo vya...

More like this