DHAHABU YENYE THAMANI YA ZAIDI YA BILIONI 1.2 YAKAMATWA IKITOROSHWA

Na Mwandishi Wetu

KUFUATIA kuimarishwa kwa mfumo wa udhibiti wa biashara haramu ya madini unaofanywa na Wizara ya Madini kupitia Kikosi Kazi (Taskforce), madini aina ya dhahabu Gramu 4,402.20 yenye thamani ya 1,238,458,594.42 yamekatwa yakitoroshwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 27 Julai, 2026 na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema Serikali kupitia Wizara ya Madini iliunda Kikosi kazi ambacho kinahusisha vyombo vya dola ili kudhibiti biashara haramu ya madini na utoroshaji.

“Hii ni sehemu tu ya kazi ambazo zimeendelea kufanywa na Kikosi kazi hicho katika kuimarisha mfumo wa ufanyaji biashara ya madini. Ndugu zangu, dhahabu hii yenye zaidi ya thamani ya bilioni 1.2 haikupitia katika mfumo rasmi wa ufanyaji biashara ya madini na hivyo kupelekea Serikali kukosa mapato ambayo yangeisaidia kuimarisha utoaji wa huduma mbalimbali kwa wananchi” alisema Mavunde.

Alibainisha kuwa dhahabu hiyo iliyokamatwa imetaifishwa kwa mujibu wa taratibu za Sheria na imehifadhiwa Benki Kuu ya Tanzania.

Vilevile, Mavunde amekielekeza Kikosi Kazi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola kumhoji vizuri mtuhumiwa aliyekamatwa na dhahabu hizo kufahamu alikotoka na alikuwa anapeleka wapi, ili kuweza kutibu kabisa mzizi wa vitendo hivyo na kuvunja mnyororo wa wote wa utoroshaji.

Mavunde alisisitiza kuwa, iwapo mtuhumiwa aliyekamatwa alikuwa na leseni ya ufanyaji biashara ya madini kufutiwa leseni hiyo mara moja na kuingizwa kwenye orodha maalum ya wenye makosa (blacklisted) ili asiruhusiwe tena kufanya biashara ya madini nchini.

Katika hatua nyingine, Waziri Mavunde alitoa rai kwa wananchi wote kuzingatia na kufuata sheria na mifumo ya ufanyaji biashara ya madini ambayo imewekwa kupitia masoko ya madini na vituo vya ununuzi ambavyo vimesambaa Nchi nzima.

spot_img

Latest articles

OTR na IMF zajadili utendaji wa taasisi za umma

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amekutana na ujumbe wa Shirika la Fedha...

MAAMBUKIZI MAPYA YA VVU YAPUNGUA KUTOKA 98,754 HADI 33,511

Na Tatu Mohamed MAAMBUKIZI mapya ya Virusi vya Ukimwi (VVU) nchini yamepungua kutoka watu 98,754...

MRADI WA UPANUZI WA KITUO CHA KUPOZA UMEME DEGE KUIMARISHA HALI YA UPATIKANAJI WA UMEME KIGAMBONI

📌Wafikia Asilimia 90 katika utekelezaji wake 📌 Kukamilika Mwisho wa Mwezi Disemba 2026 Na Mwandishi Wetu...

GBT yaikaribisha BetSasa sokoni, yaitaka kuzingatia maadili

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), James Mbalwe ameikaribisha...

More like this