UJENZI WA DARAJA LA J.P MAGUFULI (KIGONGO-BUSISI) WAFIKIA 85%.

Ujenzi wa Daraja la J.P Magufuli (Kigongo – Busisi) lenye Kilometa 3.2 pamoja na Barabara unganishi ya Kilometa 1.66, linalojengwa kuunganisha Barabara Kuu ya Usagara – Sengerema – Geita katika Ziwa Victoria umefika asilimia 85 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Desemba, 2024.

Taarifa hiyo imetolewa Machi 15, 2024 Mkoani Mwanza katika ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ikiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Selemani Kakoso (Mb) ilipoambatana na Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa kukagua maendeleo ya mradi huo.

Katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Selemani Kakoso (Mb) ameeleza kuwa Kamati imeridhishwa na utekelezaji wa ujenzi wa daraja hilo na imempongeza Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha ili mradi huo ukamilike kwa muda uliopangwa.

Kakoso ameiagiza Wizara ya Ujenzi kuhakikisha anamsimamia Mkandarasi wa daraja hilo kutoa fedha zitakazokwenda kuisaidia jamii inayozunguka mradi huo ambazo zitakuwa kielelezo kwa wananchi wa Wilaya ya Sengerema na Misungwi.

Aidha ,Kakoso ameitaka Wizara ya Ujenzi kuimarisha mifumo ya ulinzi na usalama katika daraja hilo ambalo linatokana na kodi za wanachi ili liweze kudumu kwa muda wa miaka 100.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amemshukuru Mhe. Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha ambapo mpaka sasa jumla ya Shilingi Bilioni 441.3 zimetolewa kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi anayetekeleza mradi huo.

“Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anautazama sana mradi huu kipekee, amekuwa akitoa fedha kwa kila hati za Mkandarasi zinapowasilishwa na zimekuwa zikilipwa kwa wakati ili Mkandarasi asikwame kutokana na kukosekana kwa fedha”, amesema Bashugwa.

Awali akitoa taarifa ya mradi, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS), Eng. Doroth Mtenga ameeleza kuwa mradi huo unatumika kama darasa la mafunzo kwa wanafunzi na wataalamu wetu wa ndani kupata uzoefu wa kusimamia na kujenga madaraja mengine kama hayo hapa nchini.

spot_img

Latest articles

TPRB YAENDELEA KUTOA HUDUMA SABASABA, YAPOKEA MAOMBI YA USAJILI

Na Mwandishi Wetu Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB) imeendelea kutoa huduma...

EWURA CCC yatoa elimu ya matumizi sahihi ya nishati na maji Sabasaba

Na Mwandishi Wetu BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji...

Wananchi wafurika Sabasaba

Na Mwandishi Wetu MAELFU ya wananchi wameendelea kufurika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini...

FCC yatoa elimu ya ulinzi wa mlaji na ushindani wa haki Sabasaba

Na Mwandishi Wetu Tume ya Ushindani (FCC) imeendelea kutumia Maonesho ya 50 ya Kimataifa...

More like this

TPRB YAENDELEA KUTOA HUDUMA SABASABA, YAPOKEA MAOMBI YA USAJILI

Na Mwandishi Wetu Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB) imeendelea kutoa huduma...

EWURA CCC yatoa elimu ya matumizi sahihi ya nishati na maji Sabasaba

Na Mwandishi Wetu BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji...

Wananchi wafurika Sabasaba

Na Mwandishi Wetu MAELFU ya wananchi wameendelea kufurika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini...