Picha ya Rais wa Kenya, William Ruto na kiongozi wa Upinzani nchini humo, Raila Odinga wakiwa na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni imeibua mjadala mitandaoni.
Ruto alimshinda Raila katika uchaguzi uliokuwa na ushindani mkubwa baina yao. Matokeo hayo yalisababisha uhasama baina ya wanasiasa hao wawili, kabla ya kuwapo maelewano ambayo sasa yanawaweka pamoja.
Viongozi hao watatu walikutana kujadili nia ya Odinga kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU), alisema Ruto kupitia mtandao wa X.