Mashambulizi Israel| Watanzania wawili hawajulikani walipo

*Ni wanafunzi, Ubalozi waeleza

Yerusalemu, Israel

Ubalozi wa Tanzania nchini Israel unasema kuwa hauna mawasiliano naWatanzania wawili ambao wanakaa eneo la kusini ambalo limeshuhudia mapambano baina ya wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas na jeshi la Israeli.

Balozi wa Tanzania nchini Israel, Alex Kallua amelielezwa Shirika la Utangazaji la Uingereza(BBC) mapema leo Oktoba 9, kuwa mpaka leo asubuhi, ubalozi huo umekuwa na mawasiliano na Watanzania takribani 350 waliopo nchini humo kasoro wanafunzi hao wawili.

Balozi Kallua amesema: ”Tunaendelea kuwafuatilia Watanzania wawili ambao ni wanafunzi waliokuwa wanafanya mafunzo kwa vitendo ‘internship’ kusini mwa nchi hiyo. Tunafanya jitihada za kuwapata kwanza ili kufahamu walipo na hali zao.…wanafunzi wengine takribani 260 kati ya Watanzania zaidi ya 350 wako salama katika maeneo mbalimbali nchini humo na wamekuwa na mawasiliano na ubalozi,” amesema Balozi huyo.

Sambamba na hayo, balozi huyo amesema kuwa wanaendelea kufuatilia hali ya usalama nchini humo ili kuhakikisha kila Mtanzania anakuwa salama.

”Tunafuatilia kwa karibu, na tunaendelea kupata taarifa kutoka Mamlaka za Israel kuhusu hali ilivyo. Tunaendelea kufuatilia na kuwaeleza waliopo hali ilivyo,” amesema balozi huyo.

spot_img

Latest articles

Mradi wa Taza kufungua Soko jipya la biashara ya umeme Afrika

Na Mwandishi Wetu, Mbeya IMEELEZWA kuwa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya...

Maaskofu, Masheikh nyanda za juu wahimiza uchaguzi wa amani

Na Mwandishi Wetu, Mbeya VIONGOZI wa dini kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wamewataka...

SGR yapata ajali, TRC yataja chanzo

Na Mwandishi Wetu Treni ya Mwendokasi (SGR) imeacha njia yake na kupata ajali katika eneo...

More like this

Mradi wa Taza kufungua Soko jipya la biashara ya umeme Afrika

Na Mwandishi Wetu, Mbeya IMEELEZWA kuwa mradi wa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme ya...

Maaskofu, Masheikh nyanda za juu wahimiza uchaguzi wa amani

Na Mwandishi Wetu, Mbeya VIONGOZI wa dini kutoka mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wamewataka...