Wananchi wafurika Sabasaba

Na Mwandishi Wetu

MAELFU ya wananchi wameendelea kufurika katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, vinakoendelea Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara (DITF), maarufu Sabasaba, wakitumia fursa hiyo kupata huduma, elimu na kujionea bidhaa pamoja na teknolojia mbalimbali zinazooneshwa na washiriki.

Tofauti na miaka iliyopita ambapo wengi walitembelea maonesho kwa ajili ya burudani na ununuzi wa bidhaa pekee, mwaka huu wananchi wengi wameonekana kutembelea mabanda ya taasisi za Serikali na sekta binafsi kutafuta elimu, kupata ushauri na kufuatilia huduma zinazotolewa moja kwa moja.

Katika mabanda mbalimbali, wananchi walionekana wakipata huduma za usajili, ushauri wa biashara na uwekezaji, elimu kuhusu matumizi ya teknolojia, nishati safi ya kupikia, huduma za afya, hifadhi ya jamii pamoja na masuala ya ajira na maendeleo ya ujuzi.

Baadhi ya wananchi waliozungumza na mwandishi wetu walisema maonesho hayo yamekuwa fursa muhimu ya kupata huduma ambazo kwa kawaida hulazimika kuzifuata katika ofisi mbalimbali, hivyo kuwaokoa muda na gharama.

“Tumepata nafasi ya kuuliza maswali na kupata majibu ya papo kwa papo. Hii imeturahisishia kupata huduma nyingi sehemu moja,” alisema mmoja wa wananchi aliyetembelea maonesho hayo.

Washiriki wa maonesho kutoka taasisi za umma na sekta binafsi walisema mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa tangu kuanza kwa maonesho hayo, huku wengi wakionesha shauku ya kujifunza kuhusu huduma na fursa zinazotolewa.

Mbali na huduma, maonesho hayo yameendelea kuwa jukwaa la kutangaza bidhaa zinazozalishwa nchini, kuonesha ubunifu wa teknolojia, kuunganisha wafanyabiashara na wawekezaji pamoja na kufungua masoko mapya kwa wazalishaji wa ndani.

Maonesho ya 50 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam yamewakutanisha washiriki kutoka ndani na nje ya Tanzania, yakiwa na lengo la kuhamasisha biashara, uwekezaji, ubunifu na matumizi ya teknolojia katika kukuza uchumi wa nchi.

spot_img

Latest articles

TPRB YAENDELEA KUTOA HUDUMA SABASABA, YAPOKEA MAOMBI YA USAJILI

Na Mwandishi Wetu Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB) imeendelea kutoa huduma...

EWURA CCC yatoa elimu ya matumizi sahihi ya nishati na maji Sabasaba

Na Mwandishi Wetu BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji...

FCC yatoa elimu ya ulinzi wa mlaji na ushindani wa haki Sabasaba

Na Mwandishi Wetu Tume ya Ushindani (FCC) imeendelea kutumia Maonesho ya 50 ya Kimataifa...

NACTVET yahamasisha elimu ya amali, yataka wazazi kuwapeleka watoto kwenye mafunzo ya ufundi

Na Tatu Mohamed BARAZA la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi...

More like this

TPRB YAENDELEA KUTOA HUDUMA SABASABA, YAPOKEA MAOMBI YA USAJILI

Na Mwandishi Wetu Bodi ya Usajili wa Wataalam wa Mipangomiji (TPRB) imeendelea kutoa huduma...

EWURA CCC yatoa elimu ya matumizi sahihi ya nishati na maji Sabasaba

Na Mwandishi Wetu BARAZA la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Nishati na Maji...

FCC yatoa elimu ya ulinzi wa mlaji na ushindani wa haki Sabasaba

Na Mwandishi Wetu Tume ya Ushindani (FCC) imeendelea kutumia Maonesho ya 50 ya Kimataifa...