Tanzania kuvuna matrilioni kutokana na kaboni

Serikali inatarajia kupata wastani wa shilingi trilioni 2.4 kutokana na biashara ya kaboni ambazo zitachangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo amesema bungeni Dodoma kuwa kufikia Desemba 31, 2023 Serikali ilikuwa imekwishapokea maombi 35 ya miradi mbalimbali ya biashara hiyo.

“Katika miaka ya hivi karibuni kumeibuka soko huria la biashara ya kaboni ikijumuisha misitu ya asili na ya kupanda na imeanza kushamiri hapa nchini na kuonesha inaweza kuchangia kwenye pato la taifa,” amesema Dkt. Jafo.

Waziri huyo alikuwa akijibu swali la Mbunge wa Buhigwe Kavejuru Felix aliyetaka kujua biashara ya kaboni katika misitu ya asili na ya kupanda imechangia kiasi gani pato la taifa tangu iingie nchini.

Waziri Jafo amesema katika kipindi cha mwaka 2018-22 fedha zilizopokelewa kupitia miradi inayotekelezwa kwenye halmashauri mbalimbali hapa nchini inafikia shilingi bilioni 32.

Kuhusu mkakati wa utoaji elimu ya biashara hiyo, Dkt. Jafo amesema Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEM pamoja na Wizara ya Maliasili na Utalii imefanya mkutano na wakuu wa mikoa na wilaya kupeleka ujumbe.

Amesema Tanzania pia imetumia fursa ya ushiriki katika Mkutano wa 28 Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Dubai, Falme za Kiarabu kutangaza biashara hiyo.

spot_img

Latest articles

Mgodi wa kihistoria wa niobium kujengwa Mbeya

Na Mwandishi Mbeya TANZANIA imepiga hatua muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na Marekani baada...

Ndejembi ataka Ewura kukagua maghala ya mafuta kuhakikisha hakuna mafuta yanayofichwa

📌Asema nchi ina usalama mkubwa wa mafuta hivyo wananchi waendelee kupata huduma muda wote 📌Timu...

Tanesco yagusa mioyo ya watoto wenye mahitaji maalum

📌Ni sehemu ya uwajibikaji wake kwa jamii 📌Yatoa misaada mbalimbali kwa vituo vitatu Dar...

 ‘Umimi’ wa viongozi unaua Jumuiya Afrika Mashariki

KATIKATI ya miaka ya 90 wakati mfumo wa vyama vingi unaota mizizi, lilitokea wazo...

More like this