Taliss – IST Swimming Championships yawavuta wenye mahitaji maalumu

Na Winfrida Mtoi


MASHINDANO ya mchezo wa kuogelea ‘Taliss -IST Championship’ yameanza leo Februari 14, 2026. yakishirikisha jumla ya vilabu 17, kutoka ndani na nje ya Tanzania, ikiwamo pia watu wenye mahitaji maalumu.

Michuano hiyo ya siku mbili iliyoandaliwa na klabu ya kuogelea ya Taliss- IST, inafanyika kwenye bwawa la Shule ya Kimataifa Tanganyika(IST), Masaki jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia mashindano hayo kocha wa klabu ya Taliss, Alex Mwaipasi amesema ni miaka 17 tangu wameanzisha michuano hiyo na mwaka huu umekuwa na utofauti mkubwa kwani ni mara ya kwanza wanahusisha watu wenye mahitaji maalumu.

“Kitu cha pekee kwenye mashindano haya ni kwamba tuna wenzetu wenye mahitaji maalumu, tumefanya hivi ili kuleta usawa kwenye michezo kwa sababu hawa vijana hawajazoea kuona wenzao wenye changamoto kwa kuwa ngazi ya kimataifa wanakuwa na michezo yao”

“Mwaka huu umekuwa wa mafanikio makubwa, tumefanikiwa kuleta jumla ya vilabu 17, viwili vinatokea Malawi, kimoja Rwanda na nyingine ni kutoka hapa nyumbani ikiwemo Zanzibar,” amesema Mwaipasi.

Kwa upande wake kocha anayefundisha watu wenye mahitaji maalumu, Anthony Josias, amesema wameomba kushiriki mashindano hayo kutokana na mara nyingi vijana hao kukosa nafasi ya kuwepo katika mashindano ya kuogelea.

“Leo nimekuja nao wawili lakini kwa ujumla kwenye timu wapo sita. Lengo ni kutaka kuonesha kuwa na wao ni sehemu ya jamii na kuondokana na dhana kuwa hawawezi,” ameeleza Anthony.

spot_img

Latest articles

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...

Wabunge walifuata mkumbo kwenda Morocco kuishangilia Serengeti Boys lawakuta jambo

Na Mwandishi Wetu SPIKA wa Mbunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametoa siku nne za...

More like this

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...