Msimu wa pili mbio za Pande Marathon kuzinduliwa Feb 14 Siku ya Wapendanao

Na Mwandishi Wetu

UZINDUZI wa mbio za Msakuzi Pande Game Reserve Marathon awamu ya pili, zinazofanyika ndani ya Pori la Akiba la Pande, unatarajia kufanyika Februari 14, 2026 siku ya Wapendanao (Valentine Day).

Uzinduzi huo unaondaliwa na Msakuzi Sports Promotion, unatarajiwa kufanyika kwenye ukumbi wa Forest Park Kamsuti, uliopo Mbezi Msakuzi, jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa Msakuzi Sports Promotion Filbert Mosha amewaambia Waandishi wa Habari kwamba siku ya uzinduzi kutakuwa na burudani ya bendi maalum ya muziki, vinywaji, nyama choma na shangwe nyingine.

“Tutakuwa na mgeni rasmi ambaye tutamtangaza baadaye. Lakini pia siku hiyo tutapata mrejesho na ushuhuda wa msimu uliopita, kutakuwa na surprise kwa Wapendanao, bendi itakuwa live kuanzia saa sita mchana hadi majogoo, kwa kifupi tutakuwa na uzinduzi wa kishindo ambao haujapata kutokea,” alisisitiza Mosha.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Msakuzi Sports Promotion, Dk. John Kisimbi alisema utakuwa uzinduzi wa aina yake hivyo wananchi wasipange kukosa.

“Mwaka jana ambao ulikuwa msimu wa kwanza, tulifanikiwa sana, washiriki zaidi ya 500 walijitokeza na baada ya mbio walipata burudani mbalimbali ya live bendi, nyama choma za pori, walipata fursa ya kuangalia wanyama na hakuna aliyetaka kuondoka, msimu huu wa pili mambo ni moto zaidi.

“Jambo kubwa ni kwamba siku ya Wapendanao, tutazindua rasmi msimu wa pili wa maandalizi ya mbio hizo kwenye ukumbi wa Forest Park Kamsuti,” alisema Dk. Kisimbi.

Aliishukuru Mamlaka ya Usimamizi ya Wanyama Pori Tanzania (TAWA) kwa kuridhia Pande Marathon kufanyika ndani ya hifadhi hiyo kama sehemu ya kukuza utalii wa Pande na msimu huu wa pili wanatarajia kuwa na washiriki zaidi 2000.

spot_img

Latest articles

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...

Wabunge walifuata mkumbo kwenda Morocco kuishangilia Serengeti Boys lawakuta jambo

Na Mwandishi Wetu SPIKA wa Mbunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu ametoa siku nne za...

More like this

Mchezo wa kuogelea wazidi kupaa nchini, TSA  yafichua siri

Na Winfrida  Mtoi MCHEZO wa kuogelea umezidi kushika kasi nchini  kutokana na kuongezeka idadi ya...

Dkt Nchimbi atembelea banda la Tanesco

Na Mwandishi Wetu MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi...

Waogeleaji chipukizi 400 kutikisa Dar kesho

Na Mwandishi Wetu Zaidi ya waogeleaji 400 wenye umri wa miaka 6 hadi 12 wanatarajiwa...