Simba yataka Polisi iwashughulikie waliomkashfu bosi

Na Mwandishi Wetu

KLABU ya Simba imeliandikia barua Jeshi la Polisi  ili kuwachukulia hatua za kisheria wanachama na mashabiki wa klabu hiyo  waliohusika na mkutano wa kutoa kashfa na maneno yasio ya staha kwa mwekezaji wao Mohamed Dewji (Mo).

Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Klabu hiyo, Bodi ya Wakurugenzi ya Simba imesikitishwa na vitendo hivyo na kutaka wote waliohusika au kula njama za kuandaa mkutano huo  kufikishwa katika vyombo vya dola kwa makosa ya jinai.

“Bodi inasisitisha kuwa haitabariki wala kuvumilia mtu yoyote anayeharibu taswira ya klabu kwa namna yoyote ile,” imesema taarifa hiyo.

Aidha uongozi wa Simba, umetoa onyo kwa baadhi ya wanachama na mashabiki wa klabu hiyo wanaotumia nembo rasmi ya klabu bila kupata ruhusa ya moja kwa moja kutoka kwa ngazi za juu za klabu hiyo.

Umetoa wito kwa wanachama na mashabiki kuzingatia taratibu rasmi za klabu na kushirikiana kwa pamoja katika kuendeleza heshima na hadhi ya klabu.

spot_img

Latest articles

“MADEREVA TANESCO KUWENI CHACHU UTOAJI HUDUMA BORA”

📌Watakiwa kutunza vyombo vya usafiri ili kuongeza ufanisi wa huduma 📌TANESCO yanunua vyombo vya usafiri...

Sasa itoshe kuvumilia uzembe huu

WIKI iliyopita zilisambaa habari za soko jipya la kisasa la Chuini lililojengwa kwa gharama...

CRDB yazindua msimu wa nne wa Zogo Mchongo, yasisitiza elimu ya fedha na matumizi ya teknolojia kukuza uchumi

Na Tatu Mohamed BENKI ya CRDB imezindua rasmi msimu wa nne wa kipindi cha Zogo...

More like this

“MADEREVA TANESCO KUWENI CHACHU UTOAJI HUDUMA BORA”

📌Watakiwa kutunza vyombo vya usafiri ili kuongeza ufanisi wa huduma 📌TANESCO yanunua vyombo vya usafiri...

Sasa itoshe kuvumilia uzembe huu

WIKI iliyopita zilisambaa habari za soko jipya la kisasa la Chuini lililojengwa kwa gharama...