Taifa Stars yakabidhiwa bendera tayari kwa AFCON 2025

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Prof. Palamagamba Kabudi, ameiaga na kuikabidhi bendera timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kuelekea fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON 2025).

Hafla hiyo imefanyika nchini Misri ambako Taifa Stars ilikuwa kambini kujiandaa na mashindano hayo, kabla ya timu kuelekea Morocco kwa michuano hiyo inayotarajia kuanza Desemba 21.

Akizungumza wakati wa halfa hiyo, Prof. Kabudi, amekiahidi kikosi hicho ushirikiano wa kila aina katika kuhakikisha kikosi hicho kinafanya vyema katika michuano hiyo mikubwa na yenye heshima kubwa barani Afrika na  duniani kwa ujumla.

Aidha  amewahimiza Watanzania kuipenda na kuipa moyo timu yao ya Stars kwa kuwashangilia na wale watakao kuwa na nafasi kwenda kujiunga nao kwenye mechi zao zote watakazocheza huko nchini Morocco.

Katika michuano hiyo Taifa Stars ipo kundi C lenye timu za Nigeria, Tunisia na Uganda, ambapo kikosi hicho kinachonolewa na kocha Miguel Gamondi  mchezo wa kwanza kitakutana na Nigeria Desemba 21, 2025 Uwanja wa Fès Sports Complex, Morocco

spot_img

Latest articles

“MADEREVA TANESCO KUWENI CHACHU UTOAJI HUDUMA BORA”

📌Watakiwa kutunza vyombo vya usafiri ili kuongeza ufanisi wa huduma 📌TANESCO yanunua vyombo vya usafiri...

Sasa itoshe kuvumilia uzembe huu

WIKI iliyopita zilisambaa habari za soko jipya la kisasa la Chuini lililojengwa kwa gharama...

CRDB yazindua msimu wa nne wa Zogo Mchongo, yasisitiza elimu ya fedha na matumizi ya teknolojia kukuza uchumi

Na Tatu Mohamed BENKI ya CRDB imezindua rasmi msimu wa nne wa kipindi cha Zogo...

More like this

“MADEREVA TANESCO KUWENI CHACHU UTOAJI HUDUMA BORA”

📌Watakiwa kutunza vyombo vya usafiri ili kuongeza ufanisi wa huduma 📌TANESCO yanunua vyombo vya usafiri...

Sasa itoshe kuvumilia uzembe huu

WIKI iliyopita zilisambaa habari za soko jipya la kisasa la Chuini lililojengwa kwa gharama...