Bondia Mrembo apewa Mmalawi

Na Mwandishi Wetu

BONDIA Debora Mwenda maarufu Bondia Mrembo, ameahidi kuiwakilisha vizuri Tanzania dhidi ya Mariam Dick kutoka Malawi watakapokutana katika pambano la Box on Boxing Day Desemba 26,2025, Warehouse Masaki Dar es Salaam.

Akizungumza leo Novemba 26, 2025, Debora amesema itakuwa  mara yake ya kwanza  kucheza pambano la kimataifa lakini anawaahidi watanzamia kuonesha mchezo mzuri na kuibuka na ushindi wa kishindo.

“Nashukuru kwa nafasi hii niliyoipata, ya kuonesha kitu nilichonacho, nimejiandaa vyakutosha nataka kuwaonesha watanzania kuwa najua kuufanya mchezo huu hata zaidi ya mwanaume,”

Amesema hana woga wowote kwa sababu amewekeza nguvu zake zaidi katika mazoezi na kila siku zinavyokwenda anazidi kuwa bora.

‎Naye mwalimu wa bondia huyo, Dickson Tembo amesema, anaendelea na mazoezi ya kibabe,hivyo watanzania wajiandae kushangilia ushindi wa kishindo siku hiyo.

spot_img

Latest articles

“MADEREVA TANESCO KUWENI CHACHU UTOAJI HUDUMA BORA”

📌Watakiwa kutunza vyombo vya usafiri ili kuongeza ufanisi wa huduma 📌TANESCO yanunua vyombo vya usafiri...

Sasa itoshe kuvumilia uzembe huu

WIKI iliyopita zilisambaa habari za soko jipya la kisasa la Chuini lililojengwa kwa gharama...

CRDB yazindua msimu wa nne wa Zogo Mchongo, yasisitiza elimu ya fedha na matumizi ya teknolojia kukuza uchumi

Na Tatu Mohamed BENKI ya CRDB imezindua rasmi msimu wa nne wa kipindi cha Zogo...

More like this

“MADEREVA TANESCO KUWENI CHACHU UTOAJI HUDUMA BORA”

📌Watakiwa kutunza vyombo vya usafiri ili kuongeza ufanisi wa huduma 📌TANESCO yanunua vyombo vya usafiri...

Sasa itoshe kuvumilia uzembe huu

WIKI iliyopita zilisambaa habari za soko jipya la kisasa la Chuini lililojengwa kwa gharama...