Chuo cha Malya chawafunda wakufunzi wa gym

Na Winfrida Mtoi

CHUO cha Maendeleo ya Michezo Malya kinaendesha mafunzo maalum kwa wakufunzi wa gym  na makocha wa viungo ili kuwaongezea ujuzi na  kufahamu mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kufanya kazi yao kwa weledi.

Mafunzo hayo yaliyoanza Novemba 24,2025 yanayoendelea katika ukumbi wa Uwanja wa Mkapa, jijini Dar es Salaam, yanahusisha washiriki 30 kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.

Akizungumzia lengo la kutoa mafunzo hayo, Makamu wa Mwenyekiti wa Chuo hicho, Salumu Mtumbuka amesema ni kutokana na kukua kwa michezo na  maeneo ya gym ndiyo watu wengi wanapenda kwenda kufanya mazoezi.

“Tumeona tutoe mafunzo haya kwa makocha  wa viungo wa michezo yote na wataalamu wa  gmy ambao wanafundisha watu kufanya mazoezi,  hii itasaidia kutoa elimu yao kitaalamu zaidi.

“Tutaendelea kutoa mafunzo ya michezo kwa lengo ya kupata wataalum ambao wataleta maendeleo katika Taifa letu, pia nina imani elimu hii ambayo washiriki wanapatiwa itaongeza nguvu katika mazoezi yao, “ameeleza.

Kwa upande wake mshiriki wa mafunzo hayo, Peter Pingo amesema elimu aliyoipata itamuongezea ubora katika kazi yake ya kufundisha mazoezi gym.

“Naishukuru Serikali chini ya Chuo ya Malya ambao wametoa kozi hii ambayo itatuongezea weledi na ufanisi wa kazi yetu, nina imani nitakuwa bora zaidi katika kuhakikisha watu wanapata mazoezi yenye viwango vizuri, ” ameeleza.

spot_img

Latest articles

Uwanja wa Mkwakwani wafungiwa

Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeufungia Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kutumika kwa...

Tuzo za TFF za msimu wa 2024/25 zayeyuka

Na Mwandishi Wetu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa taarifa ya kuahirisha hafla ya utoaji...

Bondia Mrembo apewa Mmalawi

Na Mwandishi Wetu BONDIA Debora Mwenda maarufu Bondia Mrembo, ameahidi kuiwakilisha vizuri Tanzania dhidi ya...

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu  ajiuzulu TEF

Na Mwandishi Wetu MKURUGENZI wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bakari Machumu amejiuzulu nafasi ya makamu...

More like this

Uwanja wa Mkwakwani wafungiwa

Na Mwandishi Wetu SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limeufungia Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kutumika kwa...

Tuzo za TFF za msimu wa 2024/25 zayeyuka

Na Mwandishi Wetu Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetoa taarifa ya kuahirisha hafla ya utoaji...

Bondia Mrembo apewa Mmalawi

Na Mwandishi Wetu BONDIA Debora Mwenda maarufu Bondia Mrembo, ameahidi kuiwakilisha vizuri Tanzania dhidi ya...