Afariki kwa kuchomwa kisu kisa Simba na Yanga

Na Mwandishi Wetu

Mabishano ya  ushabiki wa  Yanga na Simba yamesababisha kifo cha mwanaume mmoja aliyefahamika  kwa jina la Evaristo Mwambogolo (28), mkulima na mkazi wa Ululu wilayani Mbozi mkoani Songwe, baada ya kuchomwa kisu kifuani na mtu aliyejulikana kama Exavery Mwaweza.

Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mkoani humo, imesema Mwambogolo alifariki dunia akiwa njiani wakati akikimbizwa Zahanati ya Iyula kwa ajili ya matibabu.

“Uchunguzi wa awali umeonesha chanzo cha tukio hilo ni ushabiki wa mpira wa timu ya Simba na Yanga kati ya marehemu na mtuhumiwa, ambapo mtuhumiwa alitumia kisu alichokuwa nacho wakati wa ugomvi huo, mara baada ya kutenda kosa hilo, alitoroka kusikojulikana, ” imesema taarifa hiyo.

Aidha, Jeshi hilo limesema linafanya msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa huyo ili akamatwe na aweze kuhukumiwa kwa mujibu wa sheria.

spot_img

Latest articles

Simba, Yanga zaondoka nchini

Na Winfrida Mtoi Timu za Simba na Yanga leo zimeondoka nchini leo kwa ajili ya...

Yanga yaendeleza ubabe kwa Simba

Na Mwandishi Wetu Yanga imeendeleza ubabe kwa Simba baada ya leo kutwaa ubingwa wa Ngao...

CRDB Foundation na GIZ wazindua mradi wa Ajira Ye2, kuzalisha zaidi ya ajira 500

Na Mwandishi Wetu TAASISI ya CRDB Bank Foundation kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la...

Taasisi za Umma zapitisha maazimio tisa ya kuimarisha ufanisi

Na Mwandishi Wetu ZAIDI ya Wenyeviti wa Bodi na Wakuu wa Taasisi za Umma 650...

More like this