e-GA YASIFU MAGEUZI YA TANESCO KATIKA UTOAJI HUDUMA KIDIGITALI

📌 Wavutiwa namna TANESCO inavyotumia teknolojia na mitandao ya kijamii kutoa huduma nzuri kwa wananchi

Na Mwandishi Wetu

WATAALAMU kutoka Mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) wameisifu TANESCO kwa mafanikio makubwa ya matumizi ya teknolojia katika utoaji huduma kwa wateja, hatua iliyochangia kuongeza ufanisi na kuwahudumia wananchi kwa haraka zaidi.

Wakizungumza wakati wa ziara katika Kituo cha miito ya simu (Call Center) Julai 23, 2026, wataalamu hao walieleza kuvutiwa na mifumo ya kidigitali inayotumiwa na TANESCO kupokea, kufuatilia na kutatua changamoto za wateja, ikiwemo matumizi ya mitandao ya kijamii kufikisha taarifa na kupokea mrejesho kwa wakati.

Kwa upande wake, Meneja wa Kituo cha Huduma kwa Wateja TANESCO, Shamu Lameck, alisema ziara hiyo ni fursa ya kubadilishana uzoefu na kuonesha hatua ambazo Shirika limefikia katika kutumia teknolojia kuboresha huduma kwa wateja.

Aliongeza kuwa kutambuliwa kwa TANESCO kama kituo cha kujifunzia na taasisi mbalimbali kunathibitisha mafanikio ya juhudi za Shirika katika kuimarisha huduma za kidigitali na kuongeza uzoefu bora kwa wateja.

Ziara ya e-GA ni sehemu ya mwendelezo wa ujio wa taasisi na wadau mbalimbali wanaotembelea Kituo cha Call Center cha TANESCO kujifunza mbinu bora za utoaji huduma kwa wananchi.

spot_img

Latest articles

TAEC YAFANYA UKAGUZI WA MATUMIZI SALAMA YA MIONZI MKOANI LINDI

Na Mwandishi Wetu KAIMU Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bwn. Natalis Linuma, amesema...

Msajili wa Hazina aitaka TANROADS kuongeza ufanisi

Na Mwandishi Wetu MSAJILI wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, leo, Septemba 18, 2026, ametoa...

TANESCO IMEJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZA EL NIÑO – MD TWANGE

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema limejipanga kukabiliana na...

MRADI WA UMEME SIMIYU KUFUNGUA FURSA ZA UWEKEZAJI NA KUCHOCHEA SHUGHULI ZA KIUCHUMI WANANCHI

📌 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mhe.Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba...

More like this