Na Mwandishi Wetu
Klabu ya Dodoma Jiji imeachana na mchezaji Ibrahim Ajibu aliyejiunga na timu hiyo msimu uliopita.
Tangu klabu hiyo imemtangaza kocha mpya, Vincent Mashami raia wa Rwanda, Ajibu anakuwa mchezaji wa nne kuachwa, wengine ni Joash Onyango, Hassan Mwaterema na Fadhil Mwinyimvua.