CCM yamtema Luhaga Mpina

Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, hatakuwa miongoni mwa wanaowania ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya jina lake kukosa katika orodha ya watia nia waliopitishwa na Kamati Kuu ya chama hicho.

Taarifa hiyo imeelezwa leo, Jumanne Julai 29, 2025, na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla, alipoweka wazi majina ya walioteuliwa kuingia kwenye mchujo wa kura za maoni.

Katika Jimbo la Kisesa, Kamati Kuu imewateua watia nia saba ambao ni: Lusingi Makanda, Silinde Mhachile, Joel Mboyi, D. Madili Sakumi, Godfrey Mbuga, Elias Mambembela na Gambamala Michael Luchuga ambapo watapigiwa kura na wajumbe wa CCM Agosti 4, 2025 ili kumpata mgombea rasmi wa chama.

Mpina, ambaye ameliongoza jimbo hilo tangu mwaka 2005, alikuwa miongoni mwa wabunge wenye msimamo mkali na waliokuwa wakitoa kauli zenye ukosoaji dhidi ya baadhi ya maamuzi ya serikali.

Aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini ikiwemo Naibu Waziri wa Muungano na Mazingira pamoja na Waziri wa Mifugo na Uvuvi kati ya mwaka 2017 hadi 2020.

Miongoni mwa matukio yaliyotikisa wakati wa ubunge wake ni pamoja na kumkosoa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, kuhusu sakata la sukari, tuhuma ambazo baadaye zilibainika kukosa ushahidi na kusababisha Mpina kupewa adhabu ya kutohudhuria baadhi ya vikao vya Bunge.

spot_img

Latest articles

Tamasha la Singeli Agosti 2 wasanii kutoa burudani ya Kimataifa

Na Winfrida Mtoi Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa,...

Maandalizi ya Mkutano Mkuu Maalum UVCCM yamekamilika

Pichani ni Viongozi wa sekretarieti ya Umoja wa Vijana CCM wakikabidhi vifaa mbalimbali wezeshi...

INEC: Hakuna atakayeachwa nyuma kwenye Uchaguzi Mkuu 2025

Na Tatu Mohamed TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imesema imeweka mazingira wezeshi...

Serikali yawataka wakuu taasisi za umma kutengeneza mazingira rafiki ya kazi

Na Mwandishi Wetu SERIKALI imewataka wakuu wa taasisi za umma kutengeneza mazingira rafiki ya...

More like this