Media Brains yaendesha mafunzo kwa wanahabari kutumia dijitali

Kampuni ya Media Brains ikishirikiana na Shirika la Konrad Adenauer Stiftung (KAS) wanaendesha mafunzo kwa waandishi wa habari mkoani Manyara ya kuwajengea uwezo wa kuandika habari katika muktadha wa kidijiti.

Mafunzo hayo ambayo ni ya kivitendo zaidi yakiwajumuisha waandishi wabobevu katika tasnia, ni ya siku mbili kuanzia Jumatatu wiki hii.

Mafunzo hayo yanalenga kuongeza wigo wa uelewa katika uandishi wa sasa unaotamalaki katika tekinolojia ya kidijiti.

Yanalenga kuwakumbusha waandishi kwamba katika dunia ya sasa hakuna mwandishi wa habari atakayeweza kutekeleza majukumu yake kama hatajikita kufahamu uandishi wa kidijiti.

Wawezeshaji wa mafunzo hayo ni pamoja na mwandishi mkongwe nchini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Media Brains, Absalom Kibanda, aliyewaeleza waandishi kuwa dunia sasa iko kidijitali zaidi hivyo ni wajibu wa kila mwandishi kutafuta ujuzi na maarifa ya kutumia tekinolojia hiyo ili kuwa na uandishi wenye tija kwa jamii.

Aidha, aliwakumbusha kuwa pamoja na mabadiliko hayo ya tekinolojia, maadili ya uandishi yanabaki vilevile ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria zinazosimamia tasnia ya habari nchini.

Naye Jesse Kwayu, Mkurugenzi wa Media Brains akitoa mafunzo hayo aliwaambia waandishi kuwa takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) katika ripoti yake ya Septemba 2025, inaonyesha kuwa watumiaji wa intaneti wamefikia million 49 , huku watumiaji wa simu janja wakiwa ni milioni 27 nchini.

Idadi hiyo ya watu inaeleza kuwa ama ni watumiaji wa vyombo vya habari kwa njia ya kidijitali au wenyewe wanawasiliana kupeana taarifa kwa mfumo wa kidijitali.

Kwayu alisema kwa maana hiyo mfumo wa upataji na upokeaji wa taarifa umebadilika sana kuwa wa kidijiti. Hali hiyo inawalazimu waandishi wa habari kujifunza kwa bidii jinsi ya kutumia tekinolojia hiyo kama wanataka kuendelea na kazi hiyo katika mazingira ya sasa nchini na duniani kote.

spot_img

Latest articles

Waziri Gwajima aipongeza Tanesco kuandaa kongamano la wanawake la Nishati Safi ya kupikia

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dorothy Gwajima...

Makofi, vigelegele vimemrarua Mwigulu Nchemba?

Na Jesse Kwayu KATIKA mfumo wa utawala ambao chimbuko la madaraka ya dola ni wananchi,...

Katibu Mkuu Uwekezaji afanya ziara Ofisi ya Msajili wa Hazina

Na Mwandishi Wetu KATIBU Mkuu wa Ofisi ya Rais – Uwekezaji, Dk. Fred Msemwa, leo...

DCEA yakamata Tani 9.93 za Dawa za Kulevya, Watuhumiwa 151 Watiwa Mbaroni

Na Tatu Mohamed  MAMLAKA ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imekamata tani...

More like this