Mhudumu wa mochwari mbaroni kwa tuhuma za kukutwa na viungo vya binadamu

Na Mwandishi Wetu

Jeshi la Polisi mkoani Kagera linawashikilia watu wawili akiwamo mhudumu wa mochwari kwa tuhuma za kukutwa na viungo vinavyohisiwa kuwa ni vya binadamu katika nyumba moja ya wageni iliyopo Kata ya Kibeta Manispaa ya Bukoba, mkoani Kagera.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda, amesema watuhumiwa hao ni Piason Mdolo (42) anayejishughulisha na kazi za uganga wa kienyeji wilayani Mbozi Mkoani Songwe na Randan Mlomo (64) ambaye ni mtumishi wa chumba cha kuhifadhi maiti katika Hospitali ya Vwawa wilayani Mbozi, mkoani Songwe.

Kamanda Chatanda ametaja baadhi ya viungo walivyokutwa navyo watuhumiwa hao kuwa ni mfupa wa taya la binadamu, kipande cha moyo wa binadamu, kipande cha sehemu za siri za mwanamke, kondo la nyuma la tumbo la uzazi pamoja na ngozi za nyoka.

Amesema mdolo alikamatwa Juni 17,2025  akiwa na viungo hivyo na alipohojiwa, alidai kuwa alihitaji kuvitumia kwa matumizi yake binafsi na kumtaja Mlomo  kuwa ndiye aliyempatia viungo hivyo.

Amesema Jeshi la Polisi mkoani Kagera linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kabla ya kuwafikisha watuhumiwa hao katika vyombo vya sheria.

Aidha, ametoa onyo kali kwa watu wote wanaojihusisha na shughuli za uganga wa jadi bila kuwa na vibali halali, akisema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ili kudhibiti vitendo vinavyohatarisha maisha ya watu na kukiuka sheria za nchi.

spot_img

Latest articles

UWT Makangarawe watoa msaada kwa watoto wenye mahitaji maalum kuelekea Siku ya Wanawake Duniani

Na Tatu Mohamed KATIKA kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, Umoja wa Wanawake...

‘Makomandoo’ wazitia hasara Simba na Yanga

Na Mwandishi Wetu KLABU za Simba na Yanga zimetozwa faini ta sh.5,000,000 kila moja kwa...

Mwamuzi aliyekataa bao la Simba Zanzibar afungiwa

Na Mwandishi Wetu MWAMUZI Kassim Mpanga Mpanga wa Dar es Salaam, amefungiwa miezi sita  kosa...

Vunjabei, Sara kuisaka heshima ya Tanzania One ulingoni

Na Winfrida Mtoi MABONDIA wa ngumi za kulipwa, Halima Ramadhani maarufu Vunjabei na Sara Alex...

More like this