Mkazi wa Magomeni Ashinda Gari Ford Ranger Kupitia Kampeni ya Tembocard ni Shwaa ya CRDB

Na Mwandishi Wetu

MKAZI wa Magomeni, Rahabu Mwambene, ameibuka mshindi wa gari aina ya Ford Ranger XLT katika droo ya tatu ya kampeni ya Tembocard ni Shwaa, iliyoandaliwa na Benki ya CRDB.

Droo hiyo imefanyika ikiwa ni ya mwisho katika kampeni hiyo ya miezi mitatu iliyozinduliwa rasmi Februari 14, 2025, ikiwa na lengo la kuwazawadia wateja wa benki hiyo kupitia matumizi ya kadi ya Tembocard.

Akizungumza wakati wa droo hiyo, Bonaventure Paul, Mkurugenzi wa Matawi wa Benki ya CRDB, amesema jumla ya washindi 30 wamepatikana tangu kuanza kwa kampeni hiyo.

“Baada ya kumaliza raundi ya kwanza tuliyowazawadia washindi 12 waliokwenda Mbuga ya Wanyama ya Serengeti wakiwa na wenzao, tuliendelea na droo ya pili iliyotoa washindi watano ambao wataenda Ulaya. Leo tunahitimisha kwa kumzawadia Rahabu Mwambene gari aina ya Ford Ranger,” amesema Bonaventure.

Ameongeza kuwa lengo la kampeni hiyo ni kurudisha kwa jamii na kuthibitisha nafasi ya Benki ya CRDB kama taasisi inayoongoza kwa ubunifu na huduma bora nchini.

“Benki hii imekuwa kiongozi nchini Tanzania kwa ubunifu na huduma za kisasa. Tunaendelea kuvumbua njia mpya za kuwagusa wateja wetu na kuwapa thamani zaidi ya kifedha,” ameongeza.

Kwa upande wake, Ahmed Ally, Balozi wa CRDB na Msemaji wa Klabu ya Simba, amesema kampeni hiyo imevutia wateja wengi, wakiwemo mashabiki wa Simba SC, na kutoa wito kwao kujiunga na benki hiyo.

“Mwana Simba usikae kinyonge, jiungeni na Benki ya CRDB. Pia niwatoe hofu wale ambao hawaamini kuhusu kampeni hizi, waelewe kuwa ni halali na hazina janja janja,” amesema Ahmed.

Kampeni ya Tembocard ni Shwaa ni sehemu ya mkakati wa Benki ya CRDB wa kusherehekea mafanikio na kukuza matumizi ya teknolojia ya kadi kwa njia ya kuvutia na yenye tija kwa wateja wake.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...