Kinyozi ahukumiwa  kifungo cha miaka 30 jela kwa kubaka mwanafunzi

Na Mwandishi Wetu

Mahakama ya Wilaya ya Kwimba imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela kinyozi wa saluni ya kiume, Lindwa Clement Balthazari (30), mkazi wa kijiji cha Malya  baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 14 kutoka Shule ya Msingi Mwakulilima.

Hukumu hiyo imesomwa leo, Juni 17, 2025, na Hakimu Mkazi Mfawidhi Ndeko Dastan katika kesi ya jinai namba 31961/2024, baada ya mahakama kuridhika na ushahidi wa upande wa Jamhuri.

Mshtakiwa alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Desemba 4, 2024, na kusomewa shtaka la kubaka na Wakili wa Serikali Juma Kiparo, ambapo alikana kutenda kosa hilo.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Lindwa alitenda kosa hilo nyumbani kwake kwa nyakati tofauti mwezi Oktoba 2024, akitumia nafasi ya kumhudumia mtoto huyo kwenye saluni yake kabla ya kumrubuni na kumbaka, kinyume na vifungu vya sheria 130(1), 130(2)(e), na 131(1) vya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 (marejeo ya 2022).

Upande wa mashtaka uliwasilisha mashahidi wanne, wakiwemo mhanga na daktari, kuthibitisha pasipo shaka tuhuma hizo. Mtuhumiwa alijitetea kuwa alimchukua binti huyo kwa lengo la kumsaidia baada ya kufukuzwa nyumbani, hoja ambayo ilitupiliwa mbali na Mahakama.

Jitihada zake za kuleta mashahidi watatu kwa ajili ya utetezi hazikufua dafu, na Mahakama ikamhukumu kifungo hicho ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.

spot_img

Latest articles

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

‘Hali ya huduma ya maji Dar, Pwani ni shwari’

Na Mwandishi Wetu WAKAZI mbalimbali wa Jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa...

Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Uchaguzi Mkuu wa 2025 ni halali

Na Mwandishi wetu MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Hamza Johari amesema kuwa, Uchaguzi Mkuu wa...

More like this