Watu tisa wafariki dunia, 44 wajeruhiwa ajali ya basi na Lori Morogoro

Na Mwandishi Wetu

Watu tisa wamefariki dunia papo hapo na wengine 44 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya Hai lenye namba za usajili T523 EKM kugongana na lori lililokuwa limebeba shehena ya sukari lenye namba za usajili T406 CZS – T804 BUB katika eneo la Lugono Melala, barabara kuu ya Morogoro–Iringa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Alex Mkama, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, amesema kuwa ilitokea majira ya alasiri ya Juni 12, 2025.

Kwa mujibu wa Ofisa Uhisiano wa  Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, Scolastica Ndunga hospitali hiyo imepokea miili ya marehemu tisa, ambapo kati ya miili hiyo, mitano ni ya wanaume na minne ni ya wanawake.

Amesema hospitali imepokea majeruhi 44, wakiwemo watu wazima 37 na watoto saba. Amesema majeruhi wengi wamepata mivunjiko na wanaendelea kupatiwa matibabu ya haraka chini ya uangalizi wa karibu wa wataalamu wa afya.

Ndunga ameongeza kuwa miili minne kati ya tisa tayari imetambuliwa na ndugu wa marehemu kupitia vitambulisho walivyokuwa navyo. Miili mingine bado haijatambuliwa na imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali hiyo, ikisubiri utambuzi na taratibu zaidi kutoka kwa familia husika.

spot_img

Latest articles

Mwakinyo kuilipia kisasi Taifa Stars dhidi ya Mnigeria kesho, Furahi apania rekodi

Na Winfrida Mtoi BONDIA wa kimataifa wa Tanzania, Hassan Mwakinyo, ameweka bayana kuwa pambano lake...

Serikali kuendelea kuwawezesha vijana kijamii, kiuchumi

Na Tatu Mohamed WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais – Maendeleo ya Vijana, Joel...

Kids Holiday Festival yawavuta mamia ya watoto, CRDB yatumia jukwaa kujenga uelewa wa fedha

Na Mwandishi Wetu BURUDANI na michezo mbalimbali vilitawala Tamasha la Kids Holiday Festival lililowakusanya...

Mambo: Demokrasia haijengwi kwa mashinikizo, vitisho

Na Mwandishi Wetu ALIYEKUWA Mgombea wa Bavicha Taifa, Masoud Mambo amesema kuwa demokrasia ya...

More like this