Dkt. Jingu: Usawa wa Kijinsia ni kipaumbele cha Serikali

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

KATIBU Mkuu wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. John Jingu amesema Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imezingatia masuala ya Usawa wa kijinsia katika nyanja mbalimbali ikiwa juhudi za Serikali katika kuleta Usawa huo katika jamii.

Dkt. Jingu ameyasema hayo Juni 11, 2025 jijini Dodoma alipokutana na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Usawa wa Jinsia (UN Women), Hodan Addou kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa afua mbalimbali nchini juu ya uwezeshaji wanawake kiuchumi.

Dkt. Jingu ameeleza kwamba Serikali inaendelea na juhudi mbalimbali kuhakikisha kwamba Jamii inaamka na kuachana na ukatili wa kijinsia ambao umekua ni kikwazo cha maendeleo kwa ujumla.

“Kuna Kampeni ya Amsha Ari inayoendelea ambayo imelenga kujenga ufahamu juu ya masuala mbambali ya kimaendeleo kwa wananchi katika mikoa yote nchini ikiwemo suala zima la kuwainua wanawake kiuchumi“ amesema Dkt. Jingu.

Aidha Dkt. Jingu amelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na ustawi wa Jinsia (UN Women) kwa kazi nzuri linalofanya katika kuunga mkono juhudi za Serikali ili kuleta usawa wa jinsia nchini na kuwaeleza kuwa wanaweza kuongeza nguvu katika kampeni hiyo ya mageuzi ya kifikra ya “Amsha Ari” ili kuweza kukuza usawa wa kijinsia nchini.

Kwa upande wake Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya Usawa wa Jinsia (UN Women) Hodan Addou ameahidi kuwa Shirika hilo litaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kupunguza na ukatili wa kijinsia na kukuza usawa wa kijinsia.

spot_img

Latest articles

Sababu za kiusalama zazuia Lissu kufikishwa mahakamani

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Magereza limeshindwa kumfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na...

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...

Taifa Stars ya Gamondi amrejesha Kelvin John

Na Mwandishi Wetu Kaimu Kocha Mkuu wa timu ya Taifa, Taifa Stars Miguel Gamondi amemrudisha...

More like this

Sababu za kiusalama zazuia Lissu kufikishwa mahakamani

Na Mwandishi Wetu Jeshi la Magereza limeshindwa kumfikisha mahakamani Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na...

ELAF yahimiza maridhiano na amani baada ya Uchaguzi Mkuu

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam TAASISI ya Everlasting Legal Aid Foundation (ELAF) imewataka Watanzania...